Audio & Video

Kumbukizi ya Miaka 19 ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere

on

Oktoba 14, 2018 ni kumbukizi ya miaka 19 tangu afariki dunia Mwasisi wa Taifa la Tanzania na mpigania Uhuru wa Tanganyika pamoja na mataifa mbalimbali barani Afrika, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Katika kumbukizi hii, Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja mkewe Mama Janeth Magufuli wamemtembelea mjane wa Mwl. Nyerere, Mama Maria Nyerere anayeishi Msasani Jijini Dar es salaam.

Mhe. Rais Magufuli amesema serikali itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa fikra na mipango mizuri aliyoiweka inatekelezwa kwa manufaa ya watanzania wote.

Hayati Mwl. Nyerere aliyezaliwa mwaka 1922, alifariki dunia Oktoba 14, 1999 akiwa nchini Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli walimtembelea mjane wa Mwl. Nyerere, Mama Maria Nyerere nyumbani Msasani Jijini Dar es salaam.

Mhe. Rais Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere.

Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere.

Tazama BMG Online Tv hapa chini.

Picha na Ikulu & Habari Maelezo

Recommended for you