Habari Picha

Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania asimamishwa kazi

on

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Henry Semwanza

Na Mathias Canal, Dodoma

Waziri wa Kilimo Dkt.Charles Tizeba amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Methew Mtigumwe kumsimamisha kazi mara moja Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Henry Semwanza kuanzia leo Novemba 9, 2017.

Kwa agizo hilo lililotolewa na Waziri wa Kilimo Dkt.Tizeba, Mkurugenzi huyo atatakiwa kurejea kwa mwajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.

Simwanza anasimamishwa kazi kutokana na mwenendo wake wa utendaji akiwa Msimamizi Mkuu wa Bodi ya Sukari kutoridhisha ambapo amehudumu katika nafasi hiyo akiwa Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari tangu mwaka 2011.

Recommended for you