Audio & Video

MWANZA: Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Uganda aipongeza serikali

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhe.Monica Ntege amefanya ziara katika bandari za Mwanza na kuipongeza serikali ya Rais Dkt.John Magufuli kwa juhudi zilizopo za kufufua na kuboresha bandari na reli hadi nchini humo.

Mapema kabla ya kuanza ziara hiyo, Mhe.Ntege aliyeambatana na Mhandisi Dkt.Leonard Chamuriho ambaye ni Katibu Mkuu Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania alifanya mazungumzo mafupi na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia), akisalimiana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhe.Monica Ntege (kushoto) baada ya kuwasili ofisini kwake. Katikati ni Mhandisi Dkt.Leonard Chamuriho ambaye ni Katibu Mkuu Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania.

RC Mongella akimkaribisha Waziri Ntege ofisini kwake.

RC Mongella amefanya mazungumzo mafupi na Waziri Ntege.

RC Mongella akimkabidhi Waziri Ntege na ujumbe wake mwongozo wa uwekezaji mkoani Mwanza.

Ziara katika bandari ya Mwanza Kaskazini kukagua Meli ya MV.Victoria ambayo iko kwenye matengenezo.

Ziara bandari ya Mwanza Kaskazini.

Ziara katika bandari ya Mwanza Kusini.

Bandari ya Mwanza Kusini

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Wiki ya Bandari 2018

Recommended for you