Audio & Video

Mfanyabiashara akamatwa na madini nyumbani kwake

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Mashaka Biteko leo amekamata madini ya vito aina Rhodilite yanayokadiriwa kuwa tani saba katika nyumba ya mchimbaji na mfanyabiashara mmoja wa madini iliyopo Kata ya Magoweko wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Aliyekamatwa na madini hayo ambayo bado thamani yake haijafahamika ni Bw.James Mnene ambaye ni mchimbaji na mmiliki wa kampuni ya madini ya JJ.Mnene & Partiners inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito katika machimbo ya Rubeho wilayani Gairo.

Hata hivyo mfanyabishara huyo amejitetea kwamba alikuwa ametunza madini hayo nyumbani kwake huku akitafuta soko na kuomba asamehewe kwani yuko tayari kufuata taratibu za biashara ya madini.

Madini hayo yakiwa nyumbani kwa mfanyabishara huyo

Mashine iliyokutwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo ambayo ilikuwa ikitumika kusagia mawe ya madini hayo

Naibu Waziri Biteko (kushoto) akizungumza baada ya kufika nyumbani kwa mfanyabishara huyo (katikati). Mfanyabiashara huyo ametiwa nguvuni kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo anatuhumiwa kukweka kulipa mapato ya serikali kwani tangu mwaka 2013 amelipa shilingi laki nne

PIA SOMA Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko afunga machimbo ya Epanko mkoani Morogoro

Recommended for you