Habari Picha

ALAZWA HOSPITALINI BAADA YA KUMEZA SIMU YENYE MSG ALIZOTUMIWA NA MCHEPUKO AKIWA NA MPENZI WAKE.

on

Binti Mmoja mwenye umri wa miaka 19 ambae kutokana na sababu
mbambali jina lake limehifadhiwa, amelazwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa
matibabu baada ya kumeza simu yake ya mkononi.

Kisa cha
binti huyo ambae ni raia wa Brazil kumeza simu hiyo kimetokana na kutumiwa msg
za kimapenzi na Mchepuko wake huku akiwa na Mpenzi wake jambo ambalo
lilimuweka katika wakati mgumu baada ya mchumba wake huyo kutaka kuichukua simu
hiyo kwa minajiri ya kusoma msg alizokuwa ametumiwa.

Kabla ya
Binti huyo kumeza simu hiyo, kulitokea mvutano mkali baina ya wawili hao ambao
ni mtu na mchumba wake, kabla ya binti huyo kuchukua maamuzi hayo magumu ya
kubugia simu yake hiyo iliyokuwa na msg za kimahaba kutoka kwa mchepuko wake.

Madaktari
wanaomtibu binti huyo wanasema kuwa bado hali yake haijatengamaa na wanaendelea
na juhudi za kuhakikisha kuwa wanaokoa uhai wake ambapo taarifa zaidi zinaeleza
kuwa huenda binti huyo akalazimika kufanyiwa upasuaji ili kufanikisha zoezi la
kuitoa simu aliyoimeza.

Ama hakika
Michepuko ni Noma Sana. Baki Njia Kuu ili kuepukana na dhahma kama hii iliyomkumba
binti huyu, ukiachilia mbali dhahma nyinginezo kama vile Magonjwa ya zinaa kama
vile maambukizi ya virusi vya Ukimwi ama Vipigo kutoka kwa wenye Mali.

 Na: George Binagi @ 99.4 Metro FM & Mtanzania Media-Kwa Hisani ya Mtandao.

Recommended for you