Habari Picha

Watumishi Tarime wasimamishwa kazi baada ya Ambulance kukamatwa na Mirungi

on

Mkurugenzi wa Halamshauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara, Elias Ntiruhungwa akizungumza na wanahabari ofisini kwake baada ya gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) la Hospitali ya Mji wa Tarime kukamatwa wilayani Bunda likiwa na dawa za kulevya aina ya Mirungi viroba 34 jana jioni.

Na Frankius Cleophace, Tarime

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Elias Ntiruhungwa amewasimamisha kazi watumishi watatu akiwemo kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Tarime baada ya gari la kubebea wagonjwa la hospitali hiyo kukamatwa wilayani Bunda likisafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi.

Waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mganga Mkuu (DM) Dr.Innocent Kweka, Kaimu Mganga Mfawidhi  Dr.Amir Kombo na Katibu wa Hospitali hiyo Rwegasira Karugwa.

“Namsimamisha kazi DMO, Mganga Mfawidhi na Katibu wa hospitali kuanzia leo hadi tutakapomaliza uchunguzi wetu ambao umeanza kubaini kwa nini gari la wagojnwa lilitumika kusafirisha madawa ya kulevya”. Amesema Ntiruhungwa.

Amesema suala hilo linafanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini dereva wa gari hilo George Matai alipataje fursa ya kusafirisha madawa ya kulevya kwa kutumia gari la wagonjwa na kusema kuwa tayari naye amesimamishwa kazi.

Gari la kubebea wagonjwa la hospitali ya wilaya ya Tarime lililokamatwa jana jioni wilayani Bunda likisafirisha mirungi

 

Recommended for you