Audio & Video

Taasisi ya APHFTA yasaidia mapambano dhidi ya Malaria

on

George Binagi-GB Pazzo @BMG

Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria mkoani Geita yameanza kuzaa matunda baada ya maambukizi ya ugonjwa huo kushuka kutoka asilimia 38.1 mwaka 2015/16 hadi asilimia 17 mwaka 2017/18.

Mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano baina ya serikali pamoja na wadau mbalimbali wa afya ikiwemo Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania (APHFTA).

Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Malaria Aprili 25, 2018 katika uwanja wa Nyankumbu Mjini Geita.

Mganga Mkuu mkoani Geita, Dr.Japhet Simeo akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Mratibu wa taasisi ya APHFTA Kanda ya Ziwa, Dr.Joyce Mwihava akitoa salamu zake wakati wa maadhimisho hayo.

Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akiwakabidhi baadhi ya akina mama vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu vinavyotolewa bure na serikali kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel (kushoto), akisalimiana na Mratibu wa taasisi ya APHFTA Kanda ya Ziwa, Dr.Joyce Mwihava (kulia).

Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel akiwa pamoja na viongozi mbalimbali.

Mkuu wa mkoa Geita akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima Malaria katika uwanja wa Nyankumbu.

Mkuu wa mkoa Geita akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima Malaria katika uwanja wa Nyankumbu.

Bonyeza HAPA Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani 2018.

 

Recommended for you