Audio & Video

Mchungaji Fungo amtoa Bambo pepo wachafu

on

Mchungaji Apostle Godfrey Fungo wa Kanisa la Life Givers lililopo Nyasaka Centre Jijini Mwanza ameendelea kufanyika Baraka katika maisha ya wana wa Adam baada ya kumponya na pepo wachafu mchekeshaji wa siku nyingi hapa nchini, Bambo.

Mchungaji Fungo ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Mtume wa Mitume alitenda muujiza huo kupitia jina la Yesu Kristo hivi karibuni Jijini Arusha alipokuwa akihudumu kwenye kanisa la KKT Chekereni.

Muda mfupi baada ya maombezi kuanza, Bambo alianguka chini yeye pamoja na baadhi ya waumini wengine na baada ya maombi kuchachamaa walifunguliwa na kushuhudia ukuu wa Mungu kwa kuwafungua.

Recommended for you