Habari Picha

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI GEITA KWA KOSA LA MAUAJI YA MWANAE MWENYE UMRI WA MIAKA MINNE. ALIANZA KUMPAKA PILIPILI MACHONI KISHA KIPIGO KILICHOSABABISHA UMAUTI WA MTOTO HUYO.

on

Kamanda Konyo

Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia Willium Kibyala (40) Mkazi wa Kijiji cha Misiri Kata ya Bugarama, Wilayani Geita kwa kosa la kumpaka pili pili machoni mwanae John Willium (4), na kumchapa viboko sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababisha kufa.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo Joseph Konyo amethibitisha jeshi hilo kumshikilia mtuhumiwa huyo muda mfupi baada ya tukio hilo lililotokea Mei 23, 2014 ambapo amesema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

“Mtoto huyu alifariki baada ya kupewa adhabu na baba yake mzazi kwa kupigwa na kupakwa pilipili, huyu mtuhumiwa tunamshikilia hadi sasa na uchunguzi zaidi wa tukio hili bado unaendelea kwa hiyo kwa taarifa nyingine tutawambia ili muujulishe umma wa Watanzania kupitia kwenu na vyombo vingine vya habari”. Alikaririwa Konyo katika mahojiano juu ya tukio hili.

Aidha, alisema baba wa mtoto huyo anadaiwa kufanya ukatili huo baada ya kumtuhumu mtoto huyo kukataa kumfungulia mlango wakati alipotoka matembezini usiku wa manane.

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika kijiji hicho wamesema kuwa mtoto huyo mtoto huyo alifariki baada ya kuchapwa fimbo mwili mzima, kupigwa ngumi na mateke, kisha kupewa adhabu ya kukimbia riadha ya kuzunguka nyumba yao usiku wa manane kabla ya kifo chake.

Mmoja wa Wananchi hao Irene Kaijage amesema kuwa baada ya mtoto huyo kumaliza adhabu hiyo alipakwa pilipili machoni na makalioni hali iliyosababisha mtoto huyo kuzidiwa na kupoteza maisha Mei 24 jioni mwaka huu.

Mmoja wa watoto wa mzazi huyo Shija Willium amesema mdogo wao alikuwa akipewa adhabu hiyo mara kwa mara na baba yao kwa madai kwamba mama yao alimbambikizia mdogo wao huyo kwani yeye hakumzaa.
Mtanzania Media: Kwa hisani ya Mitandao: