Audio & Video

Sijawahi baguliwa wala kunyanyaswa- Diwani Chadema

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Diwani wa Kata ya Uyovu wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Mhe.Yusuph Fungameza (Chadema) amesema tangu achaguliwe kuwatumikia wananchi kupitia nafasi hiyo, hawajawi kubaguliwa kwenye vikao vya halmashauri kutokana na asilimia kubwa ya madiwani kuwa wa CCM.

Mhe.Fungameza ameyasema hayo wakati akitoa salamu zake kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Bukombe, Mhe.Doto Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini, uliofanyika katika Kijiji cha Kabulima, Uyovu. Kwenye mkutano huo, takribani wanachama 10 wa Chadema walijiunga na CCM.

Recommended for you