Burudani

Baada ya uzinduzi wa Tuliza Mawimbi, mikakati ya Ebenezer Family Band hii hapa

on

Judith Ferdinand, BMG

Kwaya ya muziki wa injili ya “Ebenezer Family Band” ya Jijini Mwanza imekusudia kufanya harambee na matamasha mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Mwanza ili kuhakikisha zinapatikana fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Msemaji wa kwaya hiyo kutoka kanisa la EAGT Kiloleli chini ya Mchungaji Dkt. Jacob Mutashi, Fabian Fanuel ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya kuchipua na kuendeleza vipaji ya Famara Promotions aliyasema hayo jumapili iliyopita kwenye uzinduzi wa albamu ya Tuliza Mawimbi ambapo alisema zinahitajika shilingi milioni 500 ili kukamilisha ujenzi huo.

Alisema kwenye uzinduzi wa albamu hiyo kiasi cha shilingi milioni 100 kilipatikana na kwamba mikakati mingine ya kwaya hiyo ni kufungua studio ya kisasa kwa ajili ya muziki na video.

“Baada ya uzinduzi wa leo tunatarajia kuelekeza nguvu katika mikoa ya Geita, Shinyanga, Simiyu, Mara, Kagera, Kigoma, Tabora kabla ya kuelekea katika mikoa mbalimbali nchini”. Alisema Fanuel.

Recommended for you