Audio & Video

Balozi wa Uturuki akutana na watoto wenye ualibino

on

Picha na Sitta Tuma

Ujumbe wa taasisi ya Josephat Tornner Foundation Europe (JTFE) pamoja na shirika la Karagwe Community Based Rehabilitation Programmes (KCBRP) ulioambatana na watoto wenye ualibino, umekutana na Balozi wa Uturuki hapa nchini, Ali Davutoglu Jijini Dar es salaam.

Baada ya mazungumzo ya pamoja, balozi Davutoglu aliketi pamoja na ujumbe huo kwa ajili ya chakula cha mchana, kabla ya kuelekea kwenye mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga uliopigwa jumapili Aprili 29, 2018 katika dimba ya Taifa ambapo Simba iliibuka kifua mbele kwa goli 1-0 dhidi ya Yanga.

Watoto wenye ualibino pamoja na wachezaji wa timu za Simba na Yanga waliingia uwanjani  na kufikisha ujumbe kwa jamii ili kuondokana na imani na fikra potofu dhidi ya mauaji ya watu wenye ualibino pamoja na kuhimiza wanajamii kuwa tayari kuwalinda, kuwathamini na kuwaheshimu watu wenye ualibino.

Recommended for you