Habari Picha

Kaimu Sheikh Mkoani Mwanza aeleza vipaumbele vyake kuifikia BAKWATA Mpya

on

Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Sheikhe Hassan Kabeke akiweka saini kwenye kitabu cha wageni kwenye ofisi za baraza hilo, kwenye hafla ya kumpokea rasmi tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo. Wanaoshudia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza hilo, Amran Batenga, aliyekuwa akikaumu nafasi hiyo, Hamis Almas pamoja na Kaimu Katibu wa baraza hilo, Sina Mwagalazi.

Kaimu Sheikhe mkoani Mwanza, Sheikhe Hassan Kabeke (kushoto) akiteta jambo na mtangulizi wake, Sheikhe Hamis Almas (kulia) muda mfupi baada ya kumvisha joho.

Kaimu Sheikhe mkoani Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Mwanza, Masheikhe wa Wilaya, Kata na Misikiti ya Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.

Kaimu Sheikhe mkoani Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Mwanza, Masheikhe wa Wilaya, Kata na Misikiti ya Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza. Picha na Baltazar Mashaka

Judith Ferdinand, BMG
Baraza la Waislamu (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza limedhamiria kuwaunganisha watanzania wote ili kuendeleza umoja, mshikamano na amani katika nchini.

Kaimu Sheikhe mkoani Mwanza, Sheikhe Hassan Kabeke aliyasema hayo Oktoba 24, 2018 wakati akizungumza kwenye hafla ya kumpokea rasmi tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo hivi karibuni.

Sheikhe Kabeke ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Mwanza, alisema katika ungozi wake ataanza kwa kuwaunganisha pamoja waislamu ili wawe kitu kimoja na kutatua migogoro iliyokuwa inawasibu pamoja pamoja na watanzania kwa ujumla bila kujali itikadi zao kwa ajili ya maendeleo na amani ya nchi.

Alisema atahakikisha anajenga nguzo za kiuchumi ndani ya baraza hilo kwa kudhibiti vyanzo vya mapato vilivyopo na kubuni vyanzo vipya.

Aidha aliahidi kuimarisha mafunzo ya dini hiyo kwa kuboresha madrasa katika maeneo ya misikiti na kwamba hayo yatafanyika kwa kasi kubwa ili kuunga mkono kauli ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikhe Abubakary Zubeir ya kuwa na BAKWATA Mpya.

Kwa upande wake Naibu Mwenyekiti wa BAKWATA (akina mama) Wilaya ya Ilemela Bakwata, Hajida Omary alisema wamefarijika kumpata Kaimu Sheikh Mkoa wa Mwanza na kuahidi ushirikiano katika kuwaunganisha waislamu wote.

Naye Katibu wa Msikiti wa Raudawa ambaye ni pia Mjumbe wa BAKWATA Halmashauri ya Mkoa Mwanza, Sheikhe Abdalah Khan alisema wapo tayari kushirikiana na Kaimu Sheikh mkoa Mwanza huku akiwataka waislamu kwa pamoja washirikiane ili waweze kufikia malengo ya Mufti Mkuu nchini ya kuwaleta pamoja waumini wa dini hiyo.

 

Recommended for you