Audio & Video

Hoja zapamba moto kikao cha baraza la madiwani Misungwi

on

Na George Binagi-GB Pazzo

Baraza la robo mwaka la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, limeendelea na vikao vyake kwa kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Baraza hilo limeketi hii leo ikiwa ni siku yake ya pili na kujadili ajenda sita ikiwemo maswali ya papo kwa hapo pamoja na taarifa ya mapato ya kwa kipindi cha robo mwaka.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Misungwi, Antony Baheme amewahimiza watendaji wa halmashauri hiyo kusimamia vyema suala la ukusanyaji wa mapato ikiwemo kuwaelimisha wanaosimamia zoezi hilo ili kutambua matumizi sahihi ya mashine za kukusanyia mapato na kuiwezesha halmashauri kukusanya mapato stahiki.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke amewataka watendaji kufuatilia orodha ya baadhi ya wakulima ambao wamepata hasara kwenye zao la pamba kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo wadudu ili kuangalia namna ya kuwasamehe madeni yao kutokana na pembejeo za kilimo walizokopeshwa.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mkuu wa wilaya ya Misungwi Juma Sweda amewataka madiwani na watendaji wa halmashauri ya Misungwi kuendelea kuwahimiza wananchi kujikita kwenye suala la kilimo cha pamba, dengu pamoja na mazao mengine kulingana na msimu wa kilimo ili kuondokana na uhaba wa mazao ya chakula na biashara huku akiwaonya wanaojihusisha na uvuvi haramu kuacha mara moja kwani hatawavumilia.

Madiwani wa halmashauri hiyo wametaka kuwepo kwa ufuatiliaji wa karibu kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara, maji, umeme pamoja na malipo kwa baadhi ya Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji waliosaidia kwenye zoezi la upigaji chapa mifugo kwani baadhi yao bado hawajalipwa stahiki zao.

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti halmashauri ya Misungwi Antony Baheme, Mkurugenzi Eliurd Mwaiteleke pamoja na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Nicodemas Ihano.

Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa wilaya Misungwi, Juma Sweda akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa wilaya Misungwi, Juma Sweda akizungumza kwenye kikao hicho.

Madiwani halmashauri ya Misungwi.

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Misungwi ambapo kushoto ni Katibu wa chama hicho Latifa Malimi na kulia ni Mwenyekiti Daud Gambalu.

Watendaji mbalimbali halmashauri ya Misungwi.

Watendaji mbalimbali halmashauri ya Misungwi wakifuatilia kikao hicho.

Kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya Misungwi.

Bonyeza HAPA ufufuaji miradi ya maji Misungwi. 

Recommended for you