Audio & Video

Uzinduzi wa Baraza la Wazee Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela

on

George Binagi-GB Pazzo @BMG

Uzinduzi wa Baraza la Wazee Kata ya Mecco katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza umefanyika leo Aprili 12, 2018 ukienda sambamba na utoaji wa vitambulisho vya msamaha wa matibabu kwa wazee wa Kata hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Renatus Mulunga akimkabidhi mmoja wa wazazi wa Kata ya Mecco, kitambulisho cha msamaha wa matibabu.

Mmoja wa wazee wa Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela akipokea kitambulisho cha msamaha wa matibabu kutoka kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga.

Mstahiki Meya Renatus Mulunga (wa tatu kulia), akimpongeza Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Kata ya Mecco, Mohamed Yusuph (wa pili kulia) baada ya kuzindua rasmi baraza hilo.

Picha ya pamoja baina ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga pamoja na viongozi mbalimbali.

Recommended for you