Habari Picha

BENKI YA AZANIA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA JIJINI DAR

on

Mmoja wa wateja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo akikata keki kwa niaba ya wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe na kulia ni Meneja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo, Naiman Sabuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akizungumza na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya Azania Tawi la Kariakoo alipotembelea benki hiyo ili kuwa bega kwa bega na wateja katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuzungumzia baadhi ya bidhaa walizonazo katika benki hiyo.Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akimlisha keki Meneja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo, Naiman Sabuni kwa niaba ya wafanyakazi wa tawi hilo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akiwalisha keki baadhi wateja wa benki ya Azania tawi la Kariakoo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ambapo benki ya Azania iko bega kwa bega na wateja wao.
Mmoja wa wateja wa Benki ya Azania tawi la Kariakoo akitoa maoni yake kuhusu benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja
 Baadhi ya wateja wa benki ya Azania tawi la Tegeta wakitoa maoni yao kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe pamoja na kuishukuru benki hiyo kuwa na mfumo wa Simu uliorahisisha huduma nyingi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akiwalisha keki wateja wa benki ya Azania tawi la Tegeta wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yaliyoanza  jumatatu Oktoba 02 mwaka huu.
Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Tegeta, Geofrey Mahona akizungumza na wateja waliofika kupata huduma kwenye benki hiyo pamoja na kuwashukuru wateja hao kwa kuwa karibu na benki hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya Azania tawi la Kariakoo.
Na Geofrey Adroph 

Recommended for you