Habari Picha

Benki ya NMB yawanoa Mawakala wake Kanda ya Ziwa

on

Meneja Kanda ya Ziwa wa Benki ya NMB, Abraham Augustino (kushoto) akikabidhi cheti cha uwakala bora wa Kanda hiyo kwa Suleiman  Rwaikondo (kulia),  katika kongamano la mawakala lililofanyika Jijini Mwanza.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.

Judith  Ferdinand, BMG

Zaidi ya mawakala 200 wa NMB kutoka Kanda ya Ziwa wamepatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo katika nyanja za huduma za kibenki, kudhibiti utakatishaji fedha haramu na ulaghai, utoaji wa huduma bora kwa wateja pamoja na kukuza biashara na ujasiriamali.

Mafunzo hayo ambayo waliyapata katika kongamano la mawakala wa benki ya NMB lililofanyika jana mkoani hapa lenye lengo la kuwaongezea ujuzi hili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Akitoa mafunzo hayo Meneja Mahusiano, Kitengo cha Uwakala Makao Makuu Nehemiah Simba alisema, utakatishaji wa fedha ni mfumo ambao wahalifu wanatumia kuweka pesa ambazo ni haramu benki au kupitia mawakala, hivyo aliwataka washiriki kuacha kufanya kazi kwa mazoea  na watoe taarifa pindi watakapokuwa na  miamala ambayo wanaitilia mashaka.

Kwa upande wake Meneja  wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa Abraham Augustino alisema, mafunzo hayo yatakuwa yanafanyika kila mwaka ili kuwafanya mawakala kufanya kazi kwa ufanisi kwani lengo la kuwepo wao ni kusogeza huduma za kibenki karibu na jamii.

“Kuwawezesha mawakala kuwafungulia wateja wapya akaunti tofauti na ilivyo sasa, pamoja na kufanya kazi ya kuweka na kutoa fedha huku watumishi wa benki wao wakishughulika na utoaji mikopo,” alisema Augustino.

Alisema, kwa sasa wanamawakala 6000 nchi nzima ila malengo yao ifikapo mwaka 2020 wawe 20000,huku akiahidi kuwa benki hiyo itaabza kutoa mikopo kwao hili waweze kujiendekeza katika biashara yao pamoja na kuangalia namna ya kuwapatia bima.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa kongamano hilo, Kalunde Kafiti aliushukuru uongozi wa NMB kwa kuona umuhimu wao na kuamua kuwapatia mafunzo hayo ambapo wamewaongezea elimu ambayo ni mtaji katika shughuli na biashara zao.

Recommended for you