Audio & Video

RC John Mongella abariki shindano la Miss Mwanza 2018

on

Judith Ferdinand, BMG

Shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Mwanza “Miss Mwanza 2018” yanatarajiwa kufanyika kesho katika viunga vya Rock City Mall.

Mkurugenzi wa shindano hilo, Pamela Irengo kutoka kampuni ya Mepal Management Ltd amesema maandalizi yote yamekamilika hivyo wakazi wa Jiji la Mwanza wajitokeze kwa wingi kushuhudia ubunifu wa washiriki wa shindano hilo.

Amesema shindano hilo litashirikisha washiriki wenye sifa ikiwemo wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24, wenye elimu kuanzia kidato cha nne, ambao hawajaolewa, hawajazaa na wenye uraia wa Tanzania.

Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye shindano hilo aliwahimiza washiriki wote kuzingatia ahadi wanazozitoa ikiwemo kusaidia jamii, kutangaza vivutio vya utalii na kutoa elimu kwa vijana wengine kujitunza ili kuepukana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Washiriki wa shindano hilo walifika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza kujitambulisha na kupata baraka za RC John Mongella na sasa kinachosubiriwa ni burudani ya kumsaka mlimbwende wa shindano hilo mwaka huu.

PIA SOMA Mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone apatikana

Recommended for you