Michezo

Jogoo la shamba lawika mjini michuano ya Rock City CUP 2018

on

Judith Ferdinand, BMG

Ule usemi wa jogoo la shamba haliwiki mjini umeshindwa kujidhihirisha baada ya timu ya Morning Star kutoka Kisesa wilayani Magu kutoa kichapo cha goli 3-0 dhidi ya Nyakato Steel kutoka Manispaa ya Ilemela.

Mchezo huo ulizikutanisha timu kutoka kundi A, ambapo kila moja imecheza michezo mitatu na kubakiza mmoja ikiwa ni mwendelezo wa mechi katika michuano ya Rock City Cup 2018.

Morning Star ilifanikiwa kufuga magoli kipindi cha pili cha mchezo huo kupitia washambuliaji wake  Malulu Thomas, Emmanuel Lushanga na Galas Thobias.

Kocha wa Morning Star Willbert  Mweta alisema wamejiandaa kwa kila mechi na kwamba timu yake itaendelea kufanyia marekebisho makosa yaliyotokea kwenye mchezo huo.

Naye kocha wa Nyakato Steel  Godfrey Chapa alisema ataajiandaa na mchezo uliosalia wa hatua za makundi kwenye michuano hiyo.

Recommended for you