Audio & Video

Wanahabari Simiyu kushirikiana na Amref kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waandishi wa habari mkoani Simiyu wameeleza namna watakavyotumia elimu waliyoipata kwenye mafunzo ya siku tatu waliyopewa na shirika la Amref Health Africa, yaliyofanyika Mjini Bariadi.

Mafunzo hayo yamefikia tamati leo ambapo yalilenga kuwajengea uwezo ili wasaidie kutoa elimu ikiwemo kuwahamasisha wanawake na wanaume kuhudhuria kliniki wanapopanga kupata mtoto.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Uzazi Uzima unaotekelezwa na shirika la Amref mkoani Simiyu, ukilenga kuboresha huduma za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Mkufunzi wa mafunzo haya alikuwa Rais Mstaafu wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya. Kwa sasa Simbaya ni Mwenyekiti wa taasisi ya Africa Media Network on Health Accauntability (AMNHA) nchini Tanzania

Wanahabari wamezungumza na BMG Online TV na kueleza namna yatakavyowasaidia katika kutimiza majukumu yao

Meneja Mradi wa Uzazi na Uzima kutoka shirika la Amref, Elia Msegu akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo

Mradi wa Uzazi Uzima unalenga kupunguza vifo vya akina mama na mtoto mkoani Simiyu

Mkufunzi Dr.Sylivester Nandi kutoka taasisi ya Nutrition International akiwasilisha mada kuhusu lishe bora na uchumi wa viwanda kwenye mafunzo hayo

PIA SOMA Shirika la Amref latoa mafunzo kwa wanahabari mkoani Simiyu

Recommended for you