Audio & Video

Malengo ya wana Bujora kupata shule ya sekondari yatimia

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Bujora wilaya Magu mkoani Mwanza unaendelea vyema na mwakani shule hiyo itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Magu, Lutengano Mwalwiba anasema ujenzi huo umetokana na jitihada za wananchi wa Kata hiyo kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali ili kuhakikisha Kata hiyo mpya inapata shule baada ya kugawanywa kutoka Kata ya Kisesa na tayari imepata nambari ya usajili.

Jana Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) tawi la Mkoa wa Mwanza walitembelea shule hiyo na kuridhishwa na ujenzi wake ambapo kukamilika kwake kutatoa fursa kielimu kwa wanafunzi wa Kata ya Bujora.

Ujenzi wa jengo la maabara za masomo ya “Bilogy, Chemistry na Physics” shule ya sekondari Bujora

SOMA>>>Zahanati ya John Mongella yarahisisha huduma za afya kwa wananchi

Recommended for you