Michezo

Chama cha soka Nyamagana chaandaa Mashindano ya Watoto

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Chama cha  Mpira wa Miguu Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza (NDFA) kimeandaa mashindano ya watoto wadogo chini ya umri wa miaka 12 na 15 yanayotarajia kuanza Disemba 11 mwaka huu katika uwanja wa Nyamagana.

Akizungumza na BMG  jana, Katibu Mkuu wa NDFA, Daddy Gilbert alisema, lengo la kuanzisha mashindano hayo katika kipindi cha likizo ni kuibia vipaji  kwa  watoto  wadogo sambamba na kuvilea.

Alisema ada ya ushiriki wa mashindano hayo ni   Sh.20,000 kwa  kila  timu, hivyo mtu mwenye taasisi, vituo vya kulelea watoto wadogo  na shule mbalimbali  zenye vituo  vya michezo, wajitokeze  katika  mashindano  hayo  ya kuibua vipaji.

“Nawaomba wadau wa michezo wenye vituo vya  michezo kujitokeza kushiriki katika mashindano hayo,  kwani yana  lengo ya kuibua vipaji kwa watoto na kuvilea  ili  kukuza michezo katika  mkoa wetu  na kuonekana  nchi za jirani,  hivyo kwenye mashindano haya hakutakuwa na zawadi yoyote itakayotolewa  kwa washindi,”alisema Daddy.

Hata hivyo, aliwataka wazazi, walezi na wadau wa soka kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwaleta watoto  katika mashindano hayo kwani vipaji huibuliwa  tangu utotoni na kuwa wachezaji wazuri  baadae, na mpira ni ajira kama ilivyoa  kazi nyingine.

Recommended for you