Audio & Video

Taasisi ya APHFTA na mapambano dhidi ya Malaria mkoani Geita

on

Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania (APHFTA) kwa kushirikiana na serikali kimeendesha mafunzo kwa wadau mbalimbali wa afya mkoani Geita, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.
 
Hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kupambana na Malaria mkoani humo ulioanza kutekelezwa Januari 2017 ukitarajiwa kufikia tamati Disemba 2019. Geita ni mkoa wa pili baada ya Kigoma kwa idadi kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.
Wataalamu wa Maabara mkoani Geita wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu matumizi ya kipimo cha haraka cha kupima Malaria MRDT
Dkt. Abdallah Balla ambaye ni Mkufunzi wa Mafunzo ya MRDT kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakijibu maswali
Meneja Mradi wa kupambana na Malaria unaosimamiwa na taasisi ya APHFTA mkoani Geita, Bigeso Makenge akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Recommended for you