Habari Picha

Zaidi ya wakazi 600 kuondokana na adha ya maji Mjini Tarime

on

Na Frankius Cleophace, Tarime

Mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara Glorious Luoga amezindua mradi wa maji katika mtaa wa Magena Kata ya Nkende Mjini Tarime ambapo zaidi ya wananchi 600 wanatarajia  kunufaika na mradi huo.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Luoga aliwataka wananchi kulinda miundombinu ya maji akiagiza kamati ya maji kuhakikisha zinatoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wa maji ili kuendeleza mradi huo.

 “Kamati ya maji itakayoundwa inaweza kuweka mpango wa kila Kaya inayopata huduma ya maji inachangia shilingi elfu moja tu kwa ajili ya uendeshaji wa mradi huo”. Alisema Luoga.

Aidha Luoga aliwapongeza wakazi wa Kata ya Nkende kwa kutoa eneo la kujenga Kituo cha Afya huku akisisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuhakikisha eneo hilo linapatiwa hati miliki ili kuondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza baina ya taasisi za serikali na wananchi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Elias Ntiruhungwa alitumia fursa hiyo kuishukukuru serikali kwa kuleta kiasi cha shilingi Millioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Nkende.

Kwa upande wake Daniel Komote ambaye ni diwani wa Kata ya Nkende alisema mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni moja ambapo wananchi wamechangia shilingi laki tano huku naye akichangia shilingili milioni moja.

Recommended for you