Audio & Video

Mkurugenzi Misungwi azungumzia utekelezaji wa miradi na ukusanyaji wa mapato

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania ALAT tawi la mkoa wa Mwanza inatarajia kufanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ili kujionea utekelezaji wa miradi hiyo.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Eliurd Mwaiteleke ameyasema hayo leo Juni 06, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kubainisha kwamba ziara hiyo itaanza na kikao cha kamati tendaji Juni 11, 2018 na kufuatiwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, afya pamoja na maji kabla ya kuhitimishwa kwa kikao cha majumuisho Juni 13, 2018.

Aidha Mwaiteleke amezungumzia mikakati ya halmashauri hiyo katika ukusanyaji wa mapato ambapo hadi Mei 31 mwaka huu ilikuwa imekusanya zaidi ya shilingi Bilioni 1.503 sawa na asilimia 73 huku lengo likiwa ni kukusana zaidi ya asilimia 80 kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Mkurugenzi Misungwi, Eliurd Mwaiteleke akizungumza na wanahabari ofisini kwake

Wanahabari

Mweka Hazina halmashauri ya Misungwi (kulia).

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Ziara ya ALAT wilayani Sengerema

Recommended for you