Audio & Video

Taasisi ya Dida Vitenge Wear yawasaidia wanafunzi wa kike Jijini Mwanza

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Taasisi ya Dida Vitenge Wear ya Jijini Mwanza imegawa pedi kwa wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Luchelele ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya hedhi duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Mei 28.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Khadija Liganga amesema hatua hiyo itawasaidia kuondokana na changamoto za kukosa masomo wakati wa hedhi ambapo ametumia pia fursa hiyo pia kuwaelimisha wanafunzi wa kike namna ya kujitunza wakati wa hedhi.

Baadhi ya mabinti wa shule ya sekondari Luchelele wameishukuru taasisi hiyo kwa msaada huo na kuwahimiza wadau wengine kushirikiana na serikali kugawa pedi bure mashuleni kwani baadhi ya wanafunzi hukumbana na changamoto ya kukosa masomo wakati wa hedhi.

Mbali na wanafunzi wengine, taasisi hiyo pia imegawa pedi 385 kwa ajili ya wanafunzi 50 wa kidato cha kwanza hadi cha tatu ambao wanatoka katika familia duni ambapo imeahidi kuwasaidia hadi watakapohitimu masomo yao ya kidato cha nne.

Mkurugenzi wa taasisi ya Dida Vitenge Wear, Khadija Liganga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Luchelele Jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani yaliyofanyika jana.

Khadija Liganga akimkabidhi pedi mmoja wa wanafunzi wa Luchelele sekondari.

David George ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Community Voices In Focus inayoendesha mradi wa Binti wa Kitaa mkoani Mwanza akimkabidhi oedi mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Luchelele.

Picha ya pamoja

Wadau mbalimbali wanahimizwa kuwasaidia mabinti pedi kwani baadhi yao hukumbwa na changamoto ya kujisitiri wakati wa hedhi.

Viongozi wa taasisi ya Dida Vitenge Wear wakiteta jambo wakati wa shughuli ya kugawa pedi katika shule ya sekondari Luchelele.

Mkurugenzi wa taasisi ya Dida Vitenge Wear, Khadija Liganga (kushoto) akiteta jambo nwa mwalimu wa shule ya sekondari Luchelele.

Wanafunzi wakiongozwa na Mkuu wao wa shule Mwl.Charles Lupimo (kushoto) walipowalaki wageni wao kutoka Dida Vitenge Wear.

Kumbukumbu na mwanafunzi aliyejibu swali kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani.

Wdau nao wako makini kikazi zaidi.

Tazama habari hapa chini. 

ISOME PIA HABARI Serikali yatakiwa kusambaza bure pedi mashuleni

Recommended for you