Habari Picha

Serikali yatakiwa kuchukua hatua kwa wasiowapeleka watoto wa kike shule

on

Na Frankius Cleophace, Serengeti

Serikali imehimizwa kuwachukia hatua kali za kisheria wazazi na walezi wanaowanyima haki ya kupata elimu watoto wa kike katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Hayo yalibainishwa na mabinti wilayani humo kwenye tamasha lililoandaliwa na shirika la RIGHT TO PLAY katika Kata ya Nata lililokuwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii ili kupiga vita ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni.

Walisema kutokana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ambazo jamii imezikumbatia, mtoto wa kike hapewi haki sawa na mtoto wa kiume hususani kupata elimu hivyo wameiomba serikali kuanzia ngazi za Vitongoji, Vijiji na Kata kuwachukulia hatua kali wazazi wasiowapeleka shule watoto wa kike.

Jedilia Charles ni Mtendaji wa Kata ya Nata aliihimiza jamii kuwa jukumu la malezi bora kwa watoto hivyo wanajamii waungane pamoja kulinda na kutetea haki za watoto huku wakiondokana na ukatili kwa watoto hao.

Leah Kimaro kutoka shirika la RIGHT TO PLAY alisema shirika hilo linatumia michezo kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii ili kuondoa ukatili katika jamii  ikiwemo ukeketaji, ndoa pamoja na mimba za utotoni.

“Sisi Kama shirika tunaendelea kutoa elimu hii hususani shule za msingi lengo ni kufikisha ujumbe kupitia michezo mbalimbali ili kuondoa mila zenye madhara” Alisema Kimaro.

Wanafunzi wa Shule za Msingi Kata ya Nata, wilaya ya Serengeti mkoani Mara wakiwa katika maandamano na mabango yenye jumbe mbalimbali za kulinda na kutetea haki za mtoto katika tamasha la kutoa elimu kwa jamii ili kupinga ukatili lililoandaliwa na shirika la RIGHT TO PLAY

Maandamano yakiendelea

Jumbe mbalimbali

Wanafunzi hao wakiwa kwenye tamasha

Wanafunzi wakiimba shairi lenye ujumbe wa kupiga vita ukatili kwa mtoto wa kike

Wanafunzi hao wakiigiza jinsi watoto wa kike wanavyolazimishwa kukeketwa ili wazazi waweze kupata mali

Igizo likiendelea

Igizo

Afisa Mtendaji wa Kata ya Nata, Jedilia Charles aliyekuwa mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Juniour FC na Elephant FC kabla ya ya michuano

Timu zikichuana

Timu ya wasichana baina ya Majengo FC na Madukani FC wakichuana vikali

Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Nata, Jedilia Charles akikabidhi zawadi ya mpira kwa nahidha wa timu ya Madukani FC

Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Nata, Jedilia Charles akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya Elephant FC baada ya kushinda Juniour FC kupitia Mikwaju ya penariti

Recommended for you