Audio & Video

Filamu mpya na ya kuvutia yazinduliwa Jijini Mwanza

on

Wasanii wa filamu mkoani Mwanza wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, wakati wa warsha kwa wasanii hao iliyofanyika miaka michache iliyopita.

Judith Ferdinand, BMG

Filamu mpya ya Great Dady imezinduliwa rasmi Jijini Mwanza ikiwa imesheheni unaowaasa wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema.

Uzinduzi wa filamu hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Brayton Film Production ulifanyika jumamosi iliyopita ambapo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Brayton Kija imetayarishwa kwa kuzingatia maudhui ya kiafrika ambapo inaweza kutazama na kila mmoja katika jamii.

Naye Monica Mathias aliyeigiza kama mtoto kwenye filamu hiyo alitoa rai kwa wadau mbalimbali ikiwemo serikali kuboresha soko la filamu nchini hususani kulinda kazi za wasanii huki mwandaaji wa filamu hiyo, Edward Kumalija akibainisha kwamba hivi sasa wasanii mkoani Mwanza wanazalisha filamu zenye ubora ikiwemo filamu ya Great Dady.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, Mwenyekiti wa mtaa wa Kishili B Bulugu Kitambo aliahidi kutoa ushirikiano zaidi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha filamu hiyo inanunuliwa kwa wingi ndani na nje ya mkoa wa Mwanza.

“Tunatakiwa kuwaunga mkono wasaanii wetu wa mkoa wa Mwanza, pia ni hatua ya kujivunia wanakishili kwa kuwa na kijana huyu ambaye ametoa yenye ujumbe wa kuhakikisha familia zinawalea watoto katika makuzi bora”. Alisema Kitambo.

Kabla ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Blues Pub uliopo Kata ya Kishili wasanii waliohusika kwenye filamu ya Great Dady alifanya usafi katika soko la Kishili ikiwa ni sehemu ya kushiriki shughuli za jamii. SOMA MAFUNZO KWA WASANII WA FILAMU ZAIDI YA 300 MKOANI MWANZA 

Recommended for you