Habari Picha

Watanzania wahimizwa kuchangamkia fursa za benki ya Mkombozi

on

Mwenyekiti wa bodi ya benki ya biashara ya Mkombizi, Method Kashonda akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka wa benki hiyo uliofanyika Jijini Dar es salaam Mei 26, 2018. Alibainisha kwamba baada ya kodi, benki hiyo imefanikiwa kupata faida ya shilingi bilioni 1.44 kwa mwaka 2017 kutoka shilingi bilioni 1.05 mwaka 2016 hii ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 37.1

BMG Habari

Benki ya biashara ya Mkombozi imeendelea kujiimarisha na kutoa huduma bora kwa wateja wake baada ya kupata faida ya shilingi bilioni 1.44 kwa mwaka 2017 kutoka shilingi bilioni 1.05 mwaka 2016 hii ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 37.1

Hayo yalibainishwa juzi na Mwenyekiti wa bodi benki ya Mkombozi, Method Kashonda wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki hiyo uliofanyika Jijini Dar es salaam na hivyo kuwahimiza watanzania kujiunga na benki hiyo ili kunufaika na huduma zake.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, George Shumbusho aliwahakikishia wateja huduma bora ikiwemo mikopo na kubainisha kwamba benki inatarajia kuanza kutumia mfumo wa kimataifa wa ripoti za fedha uitwao “International Financial Report Standard (IFRS)” ili kuwahakikishia wateja huduma bora zaidi hususani mikopo yenye riba nafuu.

Kwa upande wake Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Beatus Kinyaiya aliwahimiza watanzania wakiwemo waumini wa Kanisa Katoliki kuendelea kununua kwa wingi hisa za benki ya Mkombozi ili kunufaika na gawio lake ambapo gawio la mwaka 2017 limeongeza kwa shilingi tano sawa na shilingi 25 kwa hisa moja kutoka gawio la shilingi 20 mwaka 2016.

Nao baadhi ya wanahisa wa benki ya Mkombozi waliohudhuria mkutano huo waliipongeza benki hiyo kwa utoaji wa huduma bora na kuwahimiza watanzia kujenga utamaduni wa kuwekeza katika biashara ya hisa kwani ni biashara yenye uhakika na faida kubwa kupitia gawio la faida litolewalo kila mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki ya Mkombozi, George Shumbusho akizungumzia matarajio ya benki hiyo ya kuanza kutumia mfumo wa kimataifa wa ripoti za fedha wa International Financial Report Standard (IFRS) ili kumhakikishia mteja huduma za mkopo kwa uhakika.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Mkombozi, George Shumbusho akizungumza kwenye mkutano huo.

Makamu Mwenyekiti wa bodi ya benki ya Mkombozi, Profesa Marcellina Chijoriga akizungumza kwenye mkutano huo.

Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Beatus Kinyaiya akielezea mikakati ya benki ya Mkombozi ikiwemo kuwahimiza waumini wa kanisa Katoliki kununua hisa kwa wingi ambapo gawio la mwaka 2017 limeongeza kwa shilingi tano sawa na shilingi 25 kwa hisa moja kutoka gawio la shilingi 20 mwaka 2016.

Wanahisa wa benki ya Mkombozi wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.

Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano huo.

Recommended for you