Audio & Video

Fursa za kibiashara soko jipya Butimba Jijini Mwanza

on

Ujenzi wa soko jipya la wananchi la Kanyerere Kata ya Butimba Jijini Mwanza, unaelezwa kuibua fursa zaidi kwa wafanyabiashara ambapo wakazi wa Kata hiyo wamehimiza ujenzi huo kukamilika kwa wakati.

Aidha baadhi ya wakazi hao wakiwemo Jawadu Kidunda, Pendo Mabula pamoja na Germanus Yohana, wanasema kukamilika kwa ujezi wa soko hilo kutawaondolea adha ya kutembea umbali mrefu hadi Kata jirani ya Mkuyuni ili kupata mahitaji ya msingi.

Diwani wa Kata ya Butimba Mwl.John Pambalu anabainisha kuwa ujenzi wa soko hilo ulianza mwaka 2015 kwa wananchi kupimiwa maeneo ya kujenga vibanda na maduka wao wenyewe na kwamba hadi kukamilika kwake kutakuwa na takaribani vibanda 400, maduka 240 huku zaidi ya wafanyabiashara 700 wakinufaika moja kwa moja na soko hilo.

Ingawa soko hili bado halijakamilika na kufunguliwa rasmi, lakini tayari baadhi ya wafanyabiashari wamekwisha chungulia fursa iliyopo na hivyo kuanzisha biashara mbalimbali ikizingatiwa kwamba soko hili ni tegemeo kwa zaidi ya wakazi 30,000 wa Kata ya Butimba.

BMG Habari, Pamoja Daima!

Recommended for you