Audio & Video

Wawekezaji waanza kuchangamkia Fursa za Uwekezaji mkoani Mwanza

on

BMG Habari-Pamoja Daima!

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amesema uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Mwanza, umesaidia kuvutia zaidi wawekezaji wanaotafuta fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini.

Mongella ameyasema hayo leo wakati akifungua majadiliano ya kubadilishana uzoefu baina ya mikoa inayotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiriwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP.

Alisema mpango huo uliozinduliwa mwishoni mwa mwaka jana unawasaidia wawekezaji kutambua fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani Mwanza, na hivyo kuomba uwe endelevu katika mikoa mbalimbali nchini  katika kuelekea Tanzania ya viwanda.

Inaelezwa kwamba mkoa wa Simiyu umefanikiwa kutekeleza vyema mwongozo wake wa uwekezaji, miongoni mwa mikoa mitano nchini inayotekeleza mpango huo katika awamu ya kwanza ya majaribio.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Adolf Mkenda alisema mpango wa uandaaji wa miongozo ya uwekezaji katika mikoa mbalimbali nchini unasaidia kuzitangaza kimataifa fursa za uwekezaji zilizopo nchini.

Taasisi ya tafiti za kijamii na kiuchumi ESRF kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, inatekeleza uandaaji wa mipango wa uwekezaji katika mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Morogoro pamoja na Kilimanjaro ambapo Mkurugenzi wa shirika la UNDP hapa nchini, Natalie Boucly aliahidi ushirikiano zaidi katika utekelezaji wake.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Adolf Mkenda akizungumza kwenye majadiliano hayo. Wengine ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa shirika la UNDP hapa Tanzania Natalie Boucly (kulia).

Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella na kulia ni Mkurugenzi wa shirika la UNDP hapa nchini, Natalie Boucly wakiwa kwenye majadiliano hayo.

Capt. Mkinga Kinana kutoka JKT Rwamkoma mkoani Mara akiwasilisha uzoezi wa mradi Bulamba JKT unaofadhiliwa na UNDP ambao pamoja na mambo mengine unahusisha ujenzi wa vizimba vya kufugia samaki, mashine za chakula cha samaki na elimu kwa wanajamii katika kujikita kwenye ufugaji bora wa samaki na kuondokana na uvuvi haramu pamoja na uharibifu wa mazingira kuzunguka Ziwa Victoria.

Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Adolf Mkenda, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Antony Mtaka pamoja na Mkurugenzi wa shirika la UNDP hapa nchini Natalie Boucly.

Recommended for you