Habari Picha

Hafla ya kumuaga Katibu Mkuu Mstaafu CCM yafana Jijini Dodoma

on

Wabunge wa Chama cha Mapinduzi CCM wamefanya hafla ya kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Ndg. Abdulrahman Kinana na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya Dkt.Bashiru Ally. Hafla hiyo imefanyika jana jioni Juni 19, 2018 Jijini Dodoma. Picha na Fahadin Siraji, CCM.

Wajumbe wa Sekretariet ya CCM wakiimba maalum baada ya Katibu Mkuu Mstaafu Ndg.Abdulrahman Kinana kuwasili katika hafla hiyo

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa (kulia), akisalimiana na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg.Abdulrahman Kinana (kushoto)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya wabunge wa CCM Mhe.Majaliwa Kassim akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally kwa niaba ya Kamati ya Wabunge wa CCM

Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Ndg.Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye hafla hiyo

Katibu Mkuu Dkt.Bashiru Ally akizungumza kwenye hafla hiyo

Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya wabungea wa CCM akizungumza kwenye hafla hiyo

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Job Ndugai akizungumza kwenye hafla hiyo

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kitenge aina ya Wax mke wa Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe.Stanslaus Mabula (mwenye miwani) akisalimiana na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg.Abdulrahman Kinana (kulia)

Recommended for you