Habari Picha

UMOJA WA UVCCM TAIFA WAZIBANA HALMASHAURI NCHINI

on

Na George Binagi-GBPazzo

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM umezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatekeleza vyema utoaji wa fedha za vijana za asilimia tano zinazotokana na mapato ya ndani.

Kaimu Katibu Mkuu wa umoja huo Taifa, Shaka Hamdu Shaka (pichani juu), jana alitangaza kiama kwa halmashauri zote ambazo zitakuwa hazifanyi hivyo, wakati akizungumza na wanachama na viongozi wa jumuiya mbalimbali za CCM katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Alisema halmashauri zote nchini zinapaswa kuhakikisha fedha za asilimia tano zinawafikia vijana kwa ajili ya kuwaweza kuimarisha miradi yao ya maendeleo, ambapo aliipongeza halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kutekeleza vyema mpango huo na kuitaka kuongeza ubunifu na juhudi za kukusanya mapato ili fedha hizo ziongezeke zaidi ili kuwanufaisha vijana.

“Mimi nikupongeze Mkurugenzi maana umesema zaidi ya shilingi Milioni 390 zimetolewa kwenye vikundi vya maendeleo. Katika halmashauri nilizopita nilikuta vikundi vikipewa shilingi milioni moja kwa kila kikundi, lakini nyie mmetoa milioni mbili kwa kila kikundi, kwa kweli niwapongeze sana”. Alisema Shaka.

Katika ziara hiyo, Shaka alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ya vijana ikiwemo mradi wa tofali Buswelu, mradi wa kilimo cha umwagiliaji Sangabuye ambapo alifurahishwa na miradi hiyo kwa namna inavyofanyika chachu ya maendeleo kwa vijana na kuwaagiza viongozi wa halmashauri ya Ilemela kuhakikisha vijana wanaendelea kusaidiwa katika kuimarisha miradi yao.

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, alimhakikishia Shaka kwamba ataendelea kushirikiana na vijana wote mkoani Mwanza katika nyanja za kimaendeleo  na kwamba mikakati ya kuwavuna wanachama wapya na kuwarejesha wanaohama kutoka vyama vya upinzani itaendelea kwa kasi ambapo jana wanachama 30 kutoka Chadema tawi la Nyehunge walirejea CCM.

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akizungumza kwenye ziara hiyo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye ziara hiyo

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Manspaa ya Ilemela

Diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, akijitambulisha kwenye ziara hiyo

Emmanuel Michael ambaye ni Msimamizi wa Miradi kutoka Taasisi ya The Angeline Foundation inayosimamia mradi wa tofali Buswelu. Alisema mradi huo umeajiri vijana 35, ukiwa na mashine sita ambapo thamani yake hadi sasa ni shilingi Milioni 30.

John Nzwalile ambaye ni mmoja wa viongozi wa Shina la Nyehunge akisoma taarifa ya shina hilo kabla ya kufunguliwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka.

Kiongozi wa shina la Nyehunge (kulia) akizungumza akitoa ufafanuzi wakati wa ufunguzi wa shina hilo

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akiwapokea vijana waliojiunga na CCM kutoka shina la Nyehunge

Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akisoma maandishi ya kizalendo yaliyoandikwa kwenye shina la Nyehunge baada ya kuzinduliwa jana

Katibu wa UVCCM wilayani Ilemela, Heri James akitoa ufafanuzi kwa Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, alipowasili kwenye ofisi za CCM jana

Baadhi ya wakereketwa wa CCM wilayani Ilemela

Desin Kankono ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Vijana wilayani Ilemela akiwa kwenye mapokezi ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa

Msafara wa Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa,m ukikagua eneo la mradi wa kilimo cha umwagiliaji Sangabuye

Mradi wa tofali Buswelu

Ukaguzi wa mradi wa tofali Buswelu

Baadhi ya wanachama, mabalozi na viongozi wa jumjiya za CCM wilani Ilemela wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu kwenye uwanja wa CCM Kirumba jana

Viongozi mbalimbali wa CCM

Viongozi wa Shirika la Machinga mkoani Mwanza, wakisalimiana na Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza

Leo ziara ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa inaendelea wilayani Nyamagana. Bonyeza HAPA kutazama ziara nyingine.

Recommended for you