Audio & Video

“Kiki za wanasiasa ziishie makombe ya mbuzi siyo Riadha” – Mtaka

on

Rais wa shirikisho la riadha Tanzania, Antony Mtaka amesema ni marufuku waandaji wa mbio ndefu za Marathon (Km 42) pamoja na mbio fupi za Marathon (Km 21) kuanzisha mbio za aina hiyo bila kupata kibali kutoka kwa shirikisho hilo.

Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amepiga marufuku hiyo wakati akizungumza na wanahabari jana Jijini Mwanza, huku akibainisha kwamba kumeibuka baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia mwamvuli wa riadha kuandaa mbio za Marathon na kujipatia fedha kutoka kwa wadhamini huku wakishindwa kuwalipa vyema wakimbiaji wa mbio hizo kulingana na hadhi ya mbio za Marathon.

BMG Habari-Pamoja Daima!

Recommended for you