Habari Picha

HILI NDILO AGIZO LA MAKAMU WA RAIS KWA WATENDAJI NA WAKURUGENZI WOTE HAPA NCHINI.

on

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt.Binilith Mahenge (Kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto), Akikagua Mabanda ya maonyesho ya siku ya Mazingira duniani.

Makamu
wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal amewataka Watendaji na Wakurugenzi wa
Halmashauri zote kwa kushirikiana na wadau mbalimba hapa nchini, kuhakikisha
wanasimamia utekelezaji wa sera zinazozingatia uhifadhi na Utunzaji wa
Mazingira, ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamebainishwa leo katika taarifa yake iliyosomwa na Waziri wa
nchi Ofisi ya Makamu wa Rasi anaeshughulikia Mazingira Dkt.Binilith Mahenge,
ambae amemwakilisha katika ufunguzi wa Maadhimishoa ya Siku ya Mazingira duniani
ambayo Kitaifa yanaadhimishwa Kitaifa katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza
kuanzia June 02 hadi June 05 mwaka huu.
“Tunapoadhimisha siku ya Mazingira duniani, Watendaji na
Wakurugenzi wa Halmashauri zetu tukumbuke kusimamia utekelezaji wa mambo
yafuatayo; Kampeni ya Kitaifa ya upandaji miti, inayozitaka kila halmashauri
kupanda miti isiyopungua milioni 1.5 na kuwasilisha taarifa zao Ofisi ya Makamu
wa Rais” Alisema Dkt.Mahenge.
 Amebainisha pia kusimamia utekelezaji wa Mkakati wa hatua za
haraka za kuhifadhi Mazingira ya ardhi na vyanzo vya maji wa mwaka 2006,
sanjari na Mkakati wa hatua haraka wa kuhifadhi Bahari, Ukanda wa Pwani, Mito
na Mabwawa wa mwaka 2008.
Aidha amesisitiza juu ya Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira
iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Februari 12 mwaka 2012, pamoja na Mkakati wa
Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa Mwaka 2012, utekelezaji
ambao kwa pamoja utasaidia kuhifadhi Mazingira kwa kiwango kikubwa.
Huu ndio ushindi wa Jiji la Mwanza, Jiji safi nchini mara nane mfululizo…vipi mwaka huu? tungoje…
Hatimae shughuli ilitamatishwa hivi….Ukifika katika maonyesho hakikisha unafika katika banda hili.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo
amebainisha kuwa katika kukabiliana na athari za Tabianchi, bado Mkoa wa Mwanza
unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na suala la Ukame ambao
unaathiri zoezi la uoteshaji wa miche na upandaji wa miti ambapo amezitaja Wilaya
za Kwimba, Magu na Misungwi kukumbwa na hali hiyo zaidi.
Pia amezitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na Ukataji wa
Miti holela kwa ajili ya Mkaa na Mbao, Uvuvi haramu kwa kutumia sumu, uchimbaji
holela wa madini sanjari na uvamizi wa maeneo ya mistu kwa ajili ya shughuli za
kilimo, ufugaji na makazi ya watu.
Ambapo amebainisha kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo, Mkoa
wa Mwanza umechukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na changamoto
hizo, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya Uhifadhi wa mazingira sanjari na
kuhamasisha upandaji miti pamoja na kusimamia sheria za nchi ambazo zinahimiza
juu ya utunzaji wa mazingira.
                           
Aidha Ndikilo amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Mwanza kwa
Kushirikiana vyema na Viongozi wa Jiji la Mwanza sanjari na Manispaa ya Ilemela
katika kusimamia zoezi la kufanya Usafi wa Mazingira ifikapo jumamosi ya kwanza
ya kila mwezi.
Katika Maadhimisho hayo, shughuli mbalimbali
zitafanyika ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika maeneo yote, kuhamasisha
wananchi kuhusiana na utunzaji wa mazingira kwa njia ya makongamano.
Shughuli nyinge ni kupanda miti, kuzoa
takataka, maonyesho ya utunzaji wa mazingira, kuondoa magugu maji katika ziwa
Victoria, ufugaji wa nyuki pamoja na kufanya ziara katika maeneo
yanayojishughulisha na utunzaji wa mazingira ikiwemo viwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete
anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimishao hayo, ambapo
anatarajiwa kuwakabidhi tuzo washindi mbalimbali wanaoshiriki katika Shughuli
za Utunzaji wa Mazingira, ikiwemo Tuzo ya Rais ya Kuhidhadhi vyanzo vya maji,
kupanda na kutunza miti. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kitaifa ni “ Tunza
Mazingira ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi”.