Habari Picha

Wananchi Manispaa ya Ilemela watakiwa kujitokeza zoezi la upimaji bure

on

Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa zoezi la upimaji bure wa Saratani ya Mlango wa Kizazi katika Kituo cha Afya Buzurugua, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika jana Julai 02 ambazo upimaji utaendelea hadi Julai 06, 2018.

Judith Ferdinand, BMG

Wananchi katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upimaji bure Saratani ya Mlango wa Kizazi, matiti na Virusi vya Ukimwi linalofanyika katika Vituo vya Afya Buzuruga na Sangabue.

Mganga Mkuu wilayani Ilemela, Dkt.Florian Tinuga alitoa rai hiyo jana kwenye uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika katika Kituo cha Afya Buzuruga kwa ushirikiano baina ya Madaktari Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Califonia Marekani, Chuo cha Afya Tandabuhi pamoja na diwani Kata ya Buzuruga Mhe.Richard Machemba.

Dkt. Tinuga alisema zoezi hilo linatarajiwa kufikia tamati Julai 06, 2018 likilenga kuwafikia wasichana na wanawake zaidi ya elfu moja  wenye umri kati ya miaka 15 na 49.

“Saratani ya Mlango wa Kizazi ni ugonjwa ambao husababishwa na virusi vijulikanavyo kwa jina la kitaalam Human Papiloma virus (HPV) ambapo hutokana na sababu nyingi ikiwemo kujamiiana katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, uvutaji wa sigara huku dalili huku dalili ikiwa ni pamoja na kutokwa damu ya hedhi bila mpangilio, kutoka damu baada ya kujamiana , maumivu ya mgongo, kuchoka, kupungua uzito, kupungukiwa hamu ya kula kutokwa na uchafu wa rangi ya kahawia au damu ukeni, maumivu ya miguu au kuvimba”. Alisema Dkt.Tinuga.

Naye diwani wa Kata ya Buzuruga, Richard Machemba alisema uhusiano na wanafunzi madaktari kutoka Califonia ulianza takribani miaka mitatu iliyopita ambapo mwaka juzi waliwasaidia mashine ya “Ultra Sound” katika Kituo cha Afya Buzuruga ambapo mwaka huu wamefika kutoka bure huduma ya upimaji wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwani umekuwa ugonjwa unaosumbua akina mama duniani kote.

Agnes Lucas ambaye ni mmoa wa wananchi waliojitokeza kufanyiwa uchunguzi alisema ni vyema wananchi wengine wakawa na desturi ya kufanya uchunguzi wa afya maoema ili kujua hali yao ambapo alishukuru kupata fursa hiyo ya kufanya uchunguzi bure.

Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Buzuruga, Dkt.Eugen Rutaisire akitoa maelekezo ya awali kwa wananchi kuhusiana na zoezi hilo

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Amosy Zephania (kulia), akipokea baadhi ya vifaa vya upimaji Saratani ya Mlango wa Kizazi kutoka kwa Dkt.Justine Maher ambaye ni mmoja wa mwanafunzi daktari kutoka Chuo cha Calfonia nchini Marekani. Madaktari hao wamefika Manispaa ya Ilemela kwenye zoezi la upimaji bure Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana na wanawake.

Kulia ni Diwani Kata ya Buzuruga (Chadema), Mhe.Richard Machemba akizungumza na maadhi ya madaktari kutoka chuo cha Califonia nchini Marekani waliofika Manispaa ya Ilemela kutoa bure huduma ya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana na wanawake

Recommended for you