Audio & Video

“Ili ufanikiwe mwaka huu 2018 zingatia mambo haya”-Mchungaji Kulola

on

Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya pamoja na wananchi wameendelea kufungulia katika Semina ya Neno la Mungu inayoendelea katika kanisa hilo tangu jumanne Januari 2018 hadi jumapili ijayo Februari 04,2018.

Semina hiyo chini ya Mchungaji Kiongozo Dkt.Daniel Moses Kulola na Mama Mchungaji, Mchungaji Mercy Kulola imelenga kutoa mafundisho na miongozo muhimu ya kuzingatia kwa mwaka huu 2018 ili kuyafikia mafanikio yako kwa uweza wa Mungu.

“Kwa mwaka huu unapaswa kuwa na matunda muhimu ambayo ni pamoja na Upendo, Uvumilivu, Uaminifu na Furaha ili kuyafikia mafanikio yako”. Amesisitiza Dkt.Kulola wakati wa mwendelezo wa semina hiyo ambapo maandiko yalitoka Wagalatia 5:22, Zaburi 89:33, Mithali 12:22, Mithali 20:17 na Zaburi 51:6 hivyo ni muhimu kutafuta na kuyasoma maandiko hayo.

Aidha amesisitiza kila mmoja kuwaza na kujitamkia mambo mema ya kimafanikio mwaka huu na kumuomba Mungu kumuongoza vyema katika kuyafikia mambo hayo kwa kubariki kazi za mikono yake na hatimaye kufikia mafanikio hayo mwaka huu 2018.

“Nataka uwaze mambo mema katika ndoa yako, ujana wako, ubinti wako, kazi yako, biashara zako na Mungu naye atakuwazia mema. Lakini wakati ukiwaza hayo ni vyema ukawa mwaminifu mbele za Mungu”. Amesisitiza Dk.Kulola huku maandiko yakitoka Yeremia 29:01, Ayoub 36:5, Zaburi 23:1 na Isaya 42:16.

Katika semina hiyo wenye mahitaji mbalimbali ikiwemo magonjwa waliombewa na Mungu aliwafungua hivyo watu wote wanaosumbuliwa na maudhi mbalimbali wanahimizwa kufika kwenye semina hiyo ili kuombewa ambapo semina inaanza saa 10 jioni hadi saa 12 jioni.

Mchungaji Dkt.Kulola akifanya maombezi kwa wahitaji mbalimbali.

Maombezi yakiendelea.

Watu mbalimbali walifunguliwa.

Ipo nguvu kubwa katika maombi.

Mchungaji Kulola na Mama Mchungaji Kulola wakiwa kwenye maombezi.

Maombezi yakiendelea kanisani hapo.

Mchungaji Mercy Kulola akifanya maombi ya kufunguliwa.

Kila mmoja akishiriki maombi hayo.

Kila mmoja akishiriki maombi hayo.

Wasiliana na Mchungaji Dkt.Kulola 0767 74 90 40 kwa msaada wa kiroho. Soma zaidi HAPA

Recommended for you