Audio & Video

Taasisi ya Aga Khan yakabidhi vifaa tiba wilayani Ukerewe

on

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akizungumza kwenye hafla ya kupokea vifaa vita wilayani Ukerewe vilivyotolewa na taasisi ya Aga Khan Development Network kupitia mradi wake wa kupunguza vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga (Impact Project) unaotekelezwa mkoani Mwanza. Hafla hiyo imefanyika hii leo Juni 04, 2018 katika viunga vya hospitali ya wilaya Ukerewe ambapo mradi huo unafadhiliwa na serikali ya watu wa Canada (GAC).

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella amepokea vifaa tiba kutoka taasisi ya Aga Khan Development Network (AKDN) kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga katika wilaya ya Ukerewe.

Mongella amepokea vifaa hivyo hii leo kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viunga vya hospitali ya wilaya Ukerewe na kuwataka watumishi wa afya kuvitumia vyema vifaa hivyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Vifaa hivyo vimetolewa na taasisi ya AKDN kupitia mradi wa Impact unaotekelezwa mkoani Mwanza ambapo Meneja Mradi huo Edna Seletine amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni mashine 45 za kutakasia vifaa (Sterilizer), mashine 80 za kupimia wingi wa damu (HB Machine), mashine 160 za kupimia presha (BP Machine and Stethoscope), mashine 105 za kupimia uzito wa watoto wachanga (Infant Weighing Scales), seti 80 za kuzalishia kwa njia ya kawaida (Delivery sets), drip stands 19 pamoja na simu za rufaa 50 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 174,400,400.

Aidha amesema mradi pia utasaidia ujenzi wa chumba cha upasuaji katika hospitali ya Nansio, wodi ya akina mama kupumzika baada ya kujifungua na vyumba vya huduma za kliniki katika kituo cha afya Muriti, vyumba vitatu vya kujifungulia katika zahanati za Kamati, Busumba pamoja na Ilugwa wilayani Ukerewe vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 450,732,000.

Mganga Mkuu wilayani Ukerewe, Dr.Joshua Monge amesema vita hivyo vitatumika ipasavyo ili kuhakikisha vinasaidia kutatua changamoto ya vifo vya akina mama na watoto kabla na baada ya kujifungua.

RC Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo.

Wananchi na watumishi mbalimbali wakimsikiliza RC Mongella.

Meneja Mradi wa Impact, Edna Selestine akisoma taarifa ya mradi huo.

Meneja Mradi wa Impact, Edina Selestine (kushoto) akisoma taarifa ya mradi huo ambapo vifaa tiba vilivyokabidhiwa wilayani Ukerewe vina thamani ya shilingi Milioni 174,400,400 na utatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne.

Mganga Mkuu mkoani Mwanza (kulia) akioa salamu zake kwenye hafla hiyo.

Mganga Mkuu wilayani Ukerewe, Dr. Joshua Monge akizungumza kwenye hafla hiyo.

Kaimu Katibu wa CCM mkoani Mwanza akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.

Katibu wa CCM wilayani Ukerewe akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia), akisalimiana na Meneja Mradi wa Impact Edna Selestine (kushoto) baada ya makabidhiano ya vifaa tiba.

Mkuu wa Mkoa Mwanza akimkabidhi Mganga Mkuu wilayani Ukerewe miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa.

Mkuu wa Mkoa Mwanza akisalimiana na Mganga Mkuu wilayani Ukerewe kwenye makabidhiano hayo.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Ukerewe Mhe.Estomiah Chang”ah kwenye makabidhiano hayo.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mashine 45 za kutakasia vifaa (Sterilizer), mashine 80 za kupimia wingi wa damu (HB Machine), mashine 160 za kupimia presha (BP Machine and Stethoscope), mashine 105 za kupimia uzito wa watoto wachanga (Infant Weighing Scales), seti 80 za kuzalishia kwa njia ya kawaida (Delivery sets), drip stands 19 pamoja na simu za rufaa 50 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 174,400,400

Wananchi na watumishi mbalimbali wakishuhudia hafla hiyo.

Baada ya makabidhiano hayo, msafara wa mkuu wa mkoa ulitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa maji Nebuye.

Viongozi mbalimbali kwenye ziara na Mkuu wa Mkoa Mwanza.

Viongozi mbalimbali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza.

Akiwa katika uwanja wa michezo Ukerewe, Mkuu wa Mkoa Mwanza alikutana na watoto Janeth Kuroja (kushoto) pamoja na Fatma Athuman (kulia) wenye ualibino ambapo amewakabidhi shulingi laki moja kwa ajili ya mahitaji ya shule.

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Kilele cha Ufunuo wa Matumaini Jijini Mwanza

Recommended for you