Audio & Video

Halmashauri nchini zatakiwa kwenda kujifunza Jijini Mwanza

on

Na George Binagi-GB Pazz, BMG

Halmashauri mbalimbali nchini zimeshauriwa kufika katika halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kujifunza namna bora ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya kimkakati.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.Selemani Jaffo aliyasema hayo jumapili Mei 13, 2018 alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali Jijini Mwanza.

Mhe.Jaffo alieleza kufurahishwa na mikakati pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo machinjio ya kisasa Nyakato na hivyo kushauri halmashauri nyingine nchini hususani Kinondoni kufika Jijini Mwanza kujifunza.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba alibainisha kwamba halmashauri hiyo imeazimia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kimkakati ambayo ni stendi ya mabasi Nyegezi pamoja na stendi ya malori Buhongwa ambayo itasaidia kuongeza makusanyo ya mapato ya halmashauri.

Waziri Jaffo alikagua miradi mbalimbali Jijini Mwanza ikiwemo eneo la ujenzi wa stendi ya malori Buhongwa, eneo la ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi Nyegezi, mradi wa umeme wa jua katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana Butimba, barabara ya Mulungushi, machinjio ya kisasa Igoma pamoja na ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Nyashana na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.

Mradi wa umeme wa jua katika hospitali ya wilaya Nyamagana. Mradi huu unazalisha umeme unaotolesheleza mahitaji ya hospitali na kuuza ziada nyingine Tanesco. Mradi huu wa sola uko pia City FM radio, shule ya Buhongwa na ofisi za Jiji ukigharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.

Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jaffo akimpongeza Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia) kutokana na utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo.

Msafara wa waziri Jaffo ukiongozwa na Mkurugenzi Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba, ukikagua eneo la ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi Nyegezi.

Waziri Jaffo (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia) wakati wa ziara hiyo.

Waziri Jaffo akisalimiana na diwani Kata ya Nyegenzi.

Waziri Jaffo akiagana na wananchi waliojitokeza kumlaki katika eneo la stendi ya mabasi Nyegezi.

Waziri Jaffo akisikiliza kwa makini taarifa ya utekelezaji mradi wa machinjio ya kisasa Nyakato kutoka kwa Afisa Mifugo Jijini Mwanza, Onesmo Wilson ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu.

Machinjio ya kisasa Nyakato pia inazalisha gesi asilia kwa kutumia kinyesi cha mifugo.

Zaiara ya kukagua machinjio ya kisasa Nyakato.

Eneo la machinjio ya kisasa Nyakato.

Eneo la kuzalishia gesi asilia kutokana na kinyesi cha mifugo.

Ukaguzi eneo la kuzalishia gesi asilia kutokana na kinyesi cha mifugo.

Waziri Jaffo aliwapongeza watendaji halmashauri ya Jiji la Mwanza, madiwani, mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya Nyamagana kwa utekelezaji wa mradi huu.

Waziri Jaffo akiwasiliza baadhi ya wauzaji wa mifugo ikiwemo mbuzi eneo la machinjio ya Nyakato ambapo walimuomba wapatiwe eneo jirani na machinjio hiyo kwa ajili ya shughuli zao.

Waziri Jaffo akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wadogo wa mifugo ikiwemo mbuzi.

Waziri Jaffo akizungumza na diwani Kata ya Igogo alipotembelea na kukagua barabara ya mawe Mulungushi iliyopo katika Kata hiyo.

Waziri Jaffo akisikiliza taarifa ya ujenzi wa madarasa manne katika shule ya msingi Nyashana Kata ya Mbugani.

Waziri Jaffo akikagua madarasa yaliyojengwa katika shule ya msingi Nyashana ambapo aliridhishwa na ujenzi wake na kuipongeza halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kujenga madarasa ya aina hii zaidi ya 60 katika shule mbalimbali.

Waziri Jasho pia alimpongeza diwani Kata ya Mbugani (wa pili kushoto) kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa madarasa hayo ambapo bajeti ilikuwa kujenga madarasa matatu lakini yakajengwa madarasa manne.

Waziri Selemani Jaffo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake Jijini Mwanza. 

ISOME PIA HABARI HII Ni noma mapokezi ya Waziri Jaffo katika shule ya wasichana Ngaza

Recommended for you