Audio & Video

ALAT Mwanza yachangia miradi ya elimu, yaitunuku Magu cheti cha pongezi

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) tawi la Mkoa wa Mwanza imetoa shilingili Milioni 3.8 kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji wa miradi ya elimu katika Halmashauri za Wilaya Kwimba na Sengerema.

Akikabidhi fedha hizo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri hizo, Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza, Hilali Elisha amesema shilingi Milioni mbili ni kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya Msingi Nyamatongo Wilaya Sengerema na shilingi Milioni 1.8 kuchangia ujenzi wa shule ya Msingi Kakola wilayani Kwimba.

Pia jumuiya hiyo imekabidhi cheti cha pongezi kwa Halamshauri ya Wilaya Magu kwa kuongoza katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambapo ilikusanya asilimia 106 ikifuatiwa na Halmashauri za Misungwi 80, Ukerewe 80, Jiji la Mwanza 74, Kwimba 74, Sengerema 70, Buchosa 60 na Ilemela 42.

Hayo yalijiri jana kwenye kikao cha ALAT mkoani Mwanza kilichofanyika jana wilayani Magu.

Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Magu, Lutengano Mwalwiba (kulia) akipokea cheti cha pongezi baada ya Halmashauri hiyo kuongoza katika ukusanyaji wa mapato miongoni mwa Halmashauri za Mkoa Mwanza
Mkurugenzi Halmashauri ya Kwimba, Upendo Malabeja (kushoto) akipokea hundi ya shilingi Milioni 1.8 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule ya Msingi Kakola
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema,  Magesa Mafuru (kushoto) akipokea hundi ya shilingi Milioni mbili kwa ajili ya kuchangia ujenzi bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Nyamatongo
Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza, Hilali Elisha akizungumza kwenye mkutano huo
Tazama BMG Online Tv hapa chini 

Recommended for you