Audio & Video

Jumuiya ya ALAT Mwanza yavutiwa na miradi ya maendeleo wilayani Sengerema

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania ALAT tawi la Mkoa wa Mwanza imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali maendeleo ikiwemo ya afya, elimu na maji katika halmashauri ya wilaya ya Sengerema.

Ni baada ya jumuiya hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Hilali Elisha kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kamanga, bweni la wasichana katika shule ya sekondari Nyamatongo, mradi wa maji Chamabanda-Nyantakubwa pamoja na mradi wa utengenezaji bidhaa za ngozi ikiwemo viatu.

Mwenyekiti wa Jumuia ya ALAT tawi la Mkoa wa Mwanza, Hilali Elisha (kulia), akizungumza baada ya wajumbe wa jumuiya hiyo kufanya ziara katika Kituo cha Afya Kamanga wilayani Sengerema.

Wajumbe wa Jumuiya ya ALAT tawi la mkoa wa Mwanza wamevutiwa na ujenzi wa Kituo cha Afya Kamanga ambapo pia kinasifika kwa usafi wa mazingira, huduma bora na majengo ya kuvutia.

Wajumbe wa Jumuiya ya ALAT tawi la Mwanza wkikagua mfumo wa kusafisha maji katika Kituo cha Afya Kamanga.

Mfumo wa kusafisha maji katika Kituo cha Afya Kamanga.

Ukaguzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Nyamatongo.

Ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Nyamatongo unaojengwa kwa nguvu za wananchi, halmashauri pamoja na wadau wa maendeleo.

Wajumbe wa Jumuiya ya ALAT tawi la Mwanza akiwemo Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi Eliurd Mwaiteleke (wa kwanza mbele) pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Antony Bahebe (anayefuatia) wakitoka kukagua jengo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Nyamitongo.

Wajumbe wa Jumuiya ya ALAT tawi la Mwanza wakikagua kiwanda kidogo cha bidhaa za ngozi cha kikundi cha Neema kilichopo wilayani Sengerema.

Jumuiya ya ALAT tawi la Mwanza imedhirishwa na wajasiriamali wa kikundi cha Neema walioanzisha kiwanda hiki cha bidhaa za ngozi.

Katibu wa Jumuiya ya ALAT tawi la Mwanza Chrispin Luanda (kulia) alivutiwa na bidhaa za ngozi kiwandani hapo na kufanya manunuzi.

Baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya ALAT tawi la Mwanza, Bilarmin Hilal (kulia) akifuatiwa na Dome Manyasa ambao ni madiwani kutoka halmashauri ya Misungwi wajikionea bidhaa bora za viatu vya ngozi kiwandani hapo. Tazama video hapa chini.

ISOME PIA HABARI HII Mwanza wadhamiria kufufua kwa kasi zao la pamba

Recommended for you