Audio & Video

Serikali ya Ireland yaridhishwa na utekelezaji wa miradi wilayani Misungwi

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kamati ya bunge ya hesabu za serikali ya Irelani imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Ni baada ya jana kamati hiyo ikiambatana na balozi wa Ireland hapa nchini Mhe.Paul Sherlock kufanya ziara ya kukagua miradi miradi mbalimbali inayofadhiliwa na serikali ya Ireland kupitia shirika la Irish Aid.

Miradi hiyo ni pamoja na ule unaotekelezwa na shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI, lenye ofisi zake Nyamhongolo Jijini Mwanza unaotekelezwa katika Kata kumi za halmashauri ya Misungwi.

Mwasisi na Mkurugenzi Mstaafu wa shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI, Maimuna Kanyamala (kulia), akimlaki balozi wa Ireland nchini Tanzania Paul Sherlock baada ya kuwasili katika viunga vya kanisa Katoliki Misungwi akiambatana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kutoka Ireland.

Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland ukilakiwa baada ya kuwasili wilayani Misungwi.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland iliwasili nchini kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya.

Shirika la KIVULINI ni miongoni mwa mashirika yanayotekeleza miradi yake kwa ufadhili wa serikali ya Ireland kupitia shirika la Irish Aid.

Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Mhe.Juma Sweda akilakiwa katika viunga vya Kanisa Katoliki wilayani humo.

Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali ya Ireland walifurahishwa na utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na serikali ya Ireland hapa nchini ikiwemo mradi wa kuhamasisha jamii kuondokana na vitendo vya ukatili kwa wasichana na wanawake wilayani Misungwi unaotekelezwa na shirika la KIVULINI.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland wakifuatilia matukio mbalimbali walipowasili wilayani Misungwi.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland pamoja na wenyeji wao akiwemo Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke (wa pili kushoto).

Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Mhe.Juma Sweda (wa pili kushoto), akiwa pamoja na ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland.

Mkurugenzi halmashauri ya Misungwi (wa pili kushoto), akiteta jambo na Afisa Ustawi wa jamii mkoani Mwanza (kushoto).

Mkuu wilaya ya Misungwi akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland.

Wachezaji na wapigaji wa ngoza za asili, Chapakazi Group wakitumbuiza mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland aktika viunga vya Kanisa Katoliki wilayani Misungwi.

Kamati hiyo ilivutiwa na kufurahishwa na kikundi hiki cha ngoma.

Mwasisi na Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Mama Maimuna Kanyamala akitoa taarifa fupi ya shirika hilo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland.

Wafanyakazi wa shirika la KIVULINI, akiwemo Mkurugenzi Yassin Ally (aliyesimama) wakifuatilia matukio mbalimbali baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland kuwasili wilayani Misungwi.

Mwasisi na Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Mama Maimuna Kanyamala akizungumza na BMG Habari.

Mganga Mkuu wilayani Misungwi, Dr.Zabron Masatu (kushoto), akifafanua jambo kuhusiana na Kituo cha Afya Misasi ambacho kimepata ufadhili kutoka ushirika la Irish Aid kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa wodi ya wazazi.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland ikisikiliza kwa makini taarifa ilipotembelea Kituo cha Afya Misasi wilayani Misungwi.

Mwonekano wa jengo la wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Misasi ambayo pamoja na nguvu za wananchi na serikali ya Tanzania, pia shirika la Irish Aid kutoka Ireland linachangia ujenzi wake.

Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Mhe.Juma Sweda akizungumza baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kukagua ujezi wa wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Misasi na kuhitimisha ziara yao wilayani humo.

Meneja Mradi, Miradi ya Kujenga Uwezo kutoka shirika la Amref Health Africa nchini Tanzania, Dr.Patrick Mwidunda (kushoto), akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland baada ya kutamatisha ziara yao wilayani Misungwi.

Mkuu wa wilaya ya Misungwi (katikati) pamoja na kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Ireland.

Tazama video kwa habari zaidi hapa chini. 

ISOME PIA HABARI HII Balozi wa Ireland atoa pongezi kwa shirika la KIVULINI Jijini Mwanza

Recommended for you