Audio & Video

Halmashauri ya Misungwi yapongezwa na Kamati ya Siasa Mkoa Mwanza

on

Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Mkoa Mwanza Dkt.Antony Diallo akizungumza kwenye kikao cha majumuisho baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya Misungwi. Kutoka kushoto waliokaa ni wajumbe wa Kamati hiyo, Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Misungwi Daud Gambadu na Katibu wa CCM Misungwi Latifa Malimi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa Mwanza imeipongeza halmashauri ya Wilaya Misungwi kwa utekelezaji mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama Ilani ya uchaguzi ya 2015/20 ya chama hicho inavyoelekeza.

Ni baada ya jana kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Dkt.Antony Diallo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya na maji ili kujionea utekelezaji wake.

“Niwapongeze sana watendaji wa Serikali Kuu, Serikali za Vijiji, Wilaya, wanachama wetu wa CCM na wananchi wote maaruku kama Wananzengo kwa kutekeleza vyema Ilani ya uchaguzi ambapo mmejitahidi sana kusimamia miradi tuliyotembelea”. Alipongeza Dkt.Diallo.

Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza ambaye pia ni mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe.John Mongella alisema bado kuna fursa kubwa ya kuwekeza katika sekta ya viwanda hivyo ni vyema kila mmoja akaitumia fursa hiyo ili kuongeza ajira kwa vijana, mapato ya Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja.

Katika ziara hiyo, Kamati ya Siasa Mkoa Mwanza ilikagua ujenzi wa jengo la akina mama katika Kituo cha Afya Mbarika, tenki  la maji Lutalutale kupitia mradi wa Ngaya-Mbarika, nyumba ya waalimu (nyumba moja watumishi sita) katika shule ya Sekondari Isakamawe, jengo la akina mama katika Kituo cha Afya Misasi na ujenzi wa Shule ya Msingi Issela ambapo miradi hiyo inatekelezwa kwa fedha za Serikali, wahisani pamoja na nguvu za wananchi ikiwa na thamani ya takribani shilingi bilioni tatu.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella ambaye pia ni Mjumbe Kamati ya Siasa Mkoa akizungumza kwenye kikao cha majumuisho ya ziara ya Kamati hiyo wilayani Misungwi

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella Mhe.John Mongella (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya Misungwi Mhe.Juma Sweda (kulia)

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kushoto), akiteta jambo na Mganga Mkuu wilayani Misungwi, Dr.Zabron Masatu (wa pili kulia)

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia), akimpongeza diwani wa Kata ya Kijima Mhe.Kanzaga Ezekiel (kushoto) kwa kushirikiana vyema na wananchi katika miradi mbalimbali ya maendeleo

Mtendaji Kata ya Usagara (kulia) akifafanua jambo baada ya Kamati ya Siasa Mkoa Mwanza kutembelea ujenzi wa Shule ya Msingi Issela inayojengwa kwa nguvu za wananchi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Antony Diallo na katikati ni Mwenyekiti wa CCM wilayani Misungwi Daud Ngambadu

Mkuu wa Wilaya Misungwi Mhe.Juma Sweda akizungumza kwenye kikao cha majumuisho baada ya ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa Mwanza

Ujenzi wa wodi ya Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Mbarika

Ujenzi wa wodi ya Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Misasi

Ujenzi wa nyumba ya waalimu (nyumba moja kwa ajili ya watumishi sita) katika shule ya Sekondari Isakamawe

Moja ya jengo la madarasa katika Shule ya Msingi Issela iliyogawanyika kutoka Shule ya Msingi Busagara

Kamati ya Siasa Mkoa Mwanza baada ya kukagua ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Issela

Tazama BMG Online TV hapa chini

SOMA Kamati ya Siasa yaridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Misungwi

Recommended for you