Habari Picha

Kampeni ya “Amsha Viwanda” yafanikiwa wilayani Nyamagana

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Kampeni ya Amsha Viwanda imevuka malengo katika wilaya ya Nyamagana, baada ya wajasiriamali  zaidi ya 200 kushiriki.

Kampeni hiyo ambayo imeandaliwa na Shirika la Voluntary  Service Overseas(VSO) kupitia mradi wake wa Kuwasaidia na Kuendeleza Wajasiriamali Tanzania (TLED), wakishirikiana na SIDO, TCCIA, TWCC na ofisi ya mkoa,ambayo ili fanyika kwa siku tatu katika ukumbi Wa Gandhall ikiwa na lengo la kuwakutanisha wajasiriamali na taasisi za teknolojia,serikali na fedha pamoja na kuelimishwa juu ya usimamizi wa biashara na fedha.

Akizungumzia namna kampeni hiyo ilivyofanikiwa katika wilaya ya Nyamagana, Msimamizi Mkuu wa  VSO kupitia mradi wa TLED Frank Girabi alisema wamevuka lengo kutokana na wajasiriamali  298 walijitokeza, wakati wao walilenga kuwafikia 180.

Girabi alisema, kupitia kampeni hiyo wajasiriamali wa wilaya hiyo wameku na utayari kwani wengi waneonyesha nia ya kujifunza ambapo wameweza kufahamu nini maana ya ujasiriamali, huduma gani watazipata wakitaka kuongeza ujuzi katika biashara, kupata mikopo na  kutunza fedha zao.

Pia alisema, zaidi ya wajasiriamali 100 wataunganishwa moja kwa moja na mpango wa TLED wa kuwapatia mafunzo ya awali na ya ngazi ya juu ya masoko,usimamizi wa  biashara, fedha na mazingira na kulinda afya na usalama wa watu katika maeneo wanakofanyia shughuli zao na elimu ya jinsia ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili hasa wanawake pamoja na kushirikiana  na taasisi za kifedha ambazo zimekubali kuwaunga mkono kwa kutoa mikopo kwa wale watakaopata mafunzo hayo.

Aidha, aliishukuru serikali kupitia wakuu wa mikoa kuwaunga mkono,hivyo aliomba wawasaidie kupata wataalamu zaidi kwani changamoto inayowakabili wajasiriamali wengi hawana uelewa.

Kwa upande wake  Afisa Mradi wa Shirika la  VSO Elvis Chuwa alisema, shirika hilo kupitia mradi wake wa TLED wameweza kuwaunganisha wajasiriamali wa  mkoa wa Mwanza na Shinyanga  9 katika mikopo ya fedha na 3 ya mashine(teknolojia), na masoko kupitia maonyesho mbalimbali ndani na nje ya nchi,

Hata hivyo alisema, zaidi ya  100 waliwapatia elimu ya nembo na vifungashio sambamba na kuwaunga na kampuni zinazohusika na nembo pamoja na vifungashio ndani na nje ya nchi kwa ajili ya ubora na kutangaza bidhaa zao.

Naye Meneja wa  SIDO Bakari Songwe alisema, mwitikio ulikua ni mkubwa, hivyo kampeni hiyo itakua inafanyika mara kwa mara, ili kuhakikisha wajasiriamali wanafanya vizuri katika uzalishaji wa bidhaa na biashara zao.

Vilevile mmoja wa Wajasiriamali ambao walishiriki katika kampeni hiyo ambaye ni Katibu wa Kikundi cha Kijamii Wajasiriamali Wanawake Nyakato Mwanza Anna Mwaimu alisema, kupitia kampeni hiyo imempa elimu  kupitia TLED na SIDO ambayo ataenda kuwaelimisha wanakikundi wenzie ya kuwa kuna ushindani katika biashara, hivyo wanapaswa  kuweka huhudi katika kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuendana na soko la ndani na nje ya nchi,namna ya kusimamia fedha pamoja na kuunganishwa na huduma za kifedha.

Kadhalika  Mkurugenzi Mtendaji wa Tumaini Jipya Group Mathew Lupandisha alisema, ameweza kukutanishwa na taasisi za kifedha,teknolojia na serikali ambazo zinasaidia wajasiriamali, hivyo hiyo ni fursa ya namna ya kukuza biashara, hivyo ataku balozi kwa wengine licha ya kukabiliwa na changamoto ya vifungashio.

Recommended for you