Audio & Video

Kampeni ya “Amsha Viwanda” yafika wilayani Magu

on

Judith Ferdinand, Magu

Ili kufikia uchumi wa kati, watu wanatakiwa kubadili fikra na kuanzisha viwanda kwani wajasiriamali ni wengi lakini hawana uelewa. Hii ni kutokana na watu kudhani ya kuwa kuanzisha kiwanda mpaka uwe na fedha nyingi.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Magu George Lutengano wakati akifungua warsha ya  kampeni ya amsha viwanda, iliyoandaliwa na Shirika la Voruntary Service Overseas (VSO) kupitia mradi wake wa Kuwasaidia na Kuendeleza Wajasiriamali Tanzania (TLED) wakishirikiana na SIDO, TCCIA, TWCC na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,inayofanyika wilayani humo kwa siku tatu.

“Watu wanatakiwa kubadili fikra na kuanzisha viwanda, kwani wajasiriamali ni wengi shida ni ukosefu wa elimu juu ya viwanda pamoja na urathimishaji wa bidhaa na ubora,maana soko lipo,” alisema Lutengano.

Lutengano alisema, watatumia kampeni hiyo vizuri ili kuhakikisha wanafikia uchumi wa kati,hivyo aliwataka wanamagu walioshiriki katika warsha  kupokea mafunzo hayo kwa umakini na yawe na tija kwao kwa ajili ya kuendeleza biashara zao.

Pia aliwataka wajasiriamali kutumia taasisi za mikopo kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza biashara zao sambamba na taasisi hizo kuangalia hali za wajasiriamali ili kuwapunguzia masharti.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kwa upande wake Meneja  Mradi wa TLED wa  shirika la VSO  Mwanza Nelson  Musikula alisema, mradi huo wa miaka 5 umelenga kuwawezesha watu kiuchumi na fursa za ajira, hivyo wanawaunganisha wajasiriamali   na watoa huduma mbalimbali wanaohusika katika kuendeleza biashara, masoko sambamba na  kuwapa mafunzo na ushauri.

Naye Afisa Udhibiti Ubora wa TBS mkoa wa  Mwanza Ramadhan Hassan alisema,serikali imetenga fedha kwa  ajili ya wajasiriamali wadogo  kupimiwa bidhaa pamoja na kupatiwa nembo  ya ubora ya TBS bure,ambao wamepitia SIDO kwa kuandika barua ya maombi.

Hassan alisema, bidhaa yenye nembo ya ubora inamfanya mteja kuwa na uhakika na usalama wa afya yake sambamba na mzalishaji  kuingia katika soko la ushindani.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hata hivyo Mwenyekiti wa TWCC Mwanza, Mariam Munanka alisema siri ya mafanikio katika wajasiriamali ni  kujituma na kufanya vitu kwa malengo kwani alianza na cherehani moja na sasa anazo 7  na ameajiri watu 10,pia bado anaendelea na miradi mingine ikiwemo ufugaji. wa ng’ombe wa  maziwa na kuku.

Aidha mmoja wa  wajasiriamali walioshiriki katika warsha hiyo Onesmo Paul alisema, kupitia kampeni hiyo amejifunza namna ya kuendesha biashara kwa kufuata sheria na taratibu.

Recommended for you