Audio & Video

Kampeni ya kutokomeza Ukatili Misungwi yahitimishwa kwa mafanikio

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kampeni ya wiki nane ya kutokomeza Ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, imehitimishwa hii leo Oktoba 05, 2018 katika Kata ya Nhundulu huku ikielezwa kuwa ya mafanikio makubwa.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa Julai 04, 2018 na kusimamiwa na Halmashauri ya wilaya Misungwi kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wasichana/ watoto na wanawake KIVULINI lenye ofisi zake Nyamhongolo Jijini Mwanza.

Hadi kufikia tamati, imewafikia zaidi ya wananchi elfu thelathini katika Kata 22 kati ya Kata 27 wilayani Misungwi ambapo awamu ya pili inatarajiwa kuanza tena Novemba 25, 2018 ili kukamilisha Kata zote.

Katikati ni mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya Misungwi Mhe. Juma Sweda akifurahia ngoma ya asili wakati wa kilele cha kampeni hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally.
Ngoma ya Sungusungu Mwamagili wilayani Misungwi ikitumbuiza.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi, Antony Bahebe (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Fredrick Nyoka (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia).
Tazama hapa chini BMG Online Tv 

Recommended for you