Audio & Video

KAMPUNI YA “WONDERS ENTERTAINMENT” YATANGAZA FURSA KWA WAIMBAJI

on

Na Yusuph Magupa
Mwimbaji wa muziki wa ijili Boaz Charles ambaye pia anamiliki kampuni ya Wonders Entertainment iliyopo Arusha, inayojihusisha na vijana wa kikristu wenye vipaji ametabainisha kupitia Binagi Media kuwa yuko mchakatoni kutafuta vipawa vya waimbaji wa injili wanaojua kwa nini wanaimba ili wafanye kazi katika studio zake za Wounder Music na pia atakuwa tayari kusimamia kazi hizo ili zifikie lengo la kushangaza mataifa.
Amefafanua kuwa lazima waimbaji wa injili wa nchini waimbe kwa kupanua wigo, yaani kuvuka mipaka ili kukuza injili nje ya mipaka, ameyasema hayo huku akitolea mfano waimbaji Miriam Jackson na Angela Bernad kama waimbaji mwenye miguso ya kukubalika ndani na nje ya nchi.

Katika kuelekea kwenye uzinduzi wa taasisi ya Wounder Entertainment Empire inayojihusisha na vijana wa kikristu wenye vipaji, Mkurugenz wa taasisi hiyo Boaz Charles ameanza kwa kurekodi wimbo huu. Tazama hapo chini.

Recommended for you