Audio & Video

MAONESHO YA NANE NANE, MGODI WA GGM WAWANUFAISHA WAWAKULIMA

on

Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine (GGM) uliopo mkoani Geita umetumia zaidi ya shilingi Bilioni Mbili katika kipindi cha mwaka 2015/17 katika kusaidia uzalishaji na uongezaji wa thamani kwenye mazao ya kilimo ikiwemo mpunga na alzeti.

Meneja Mahusiano ya jamii wa mgodi huo, Manace Ndoroma (pichani) ameyasema hayo kwenye Maonyesho ya Wakulima na Wafugaji Kanda ya Ziwa yanayoendelea katika uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza.

“Tumeisha tumia bilioni mbili na milioni 800 kwenye kusaidia uongezaji wa thamani kwenye mazao, uongezaji wa kiwango cha uzalishaji, lakini pia kusaidia miradi ya ujasiriamali ambayo inayohusiana na kilimo, kwa mfano tumeanzisha kikundi ambacho kimejifunza kutengeneza viatu kwa kutumia ngozi tukitarajia kwamba kwa njia hiyo ngozi itapata soko pana zaidi”.

Aidha Ndoroma amedokeza kwamba mgodi huo uko kwenye mkakati ya kusaidia uanzishwaji wa mradi wa kusindika maziwa mkoani Geita lengo ikiwa ni kuongeza thamani kwenye uuzaji wa maziwa.

“Biashara yetu kubwa ni uchimbaji wa dhahabu lakini tumesema hii dhahabu iingie kwenye njia zingine za uchumi ili kwa pamoja tushirikiane na serikali kuhakikisha kwamba tunaingia hatua ya uchumi wa kati”. Anasema Ndoroma.

Mwenyekiti wa Kilimo cha alzeti kutoka Kijiji cha Kasota mkoani Geita ameushukuru mgodi huo kwa kuwasaidia kupata elimu ya na zana za kilimo cha zao la alzeti ambapo sasa wanalima zao hilo kisasa zaidi na mavuno wayapatayo huyatumia kuzalisha mafuta ya alzeti yenye nembo ya Nyabusakama Cooking Oil.

Tazama video hapo chini

BMG Habari, Pamoja Daima!

Recommended for you