Habari Picha

SHIRIKA LA WOTESAWA LAYATUMIA VYEMA MAONESHO YA NANE NANE

on

Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani nchini WOTESAWA lenye makazi yake Jijini Mwanza, limeyatumia Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nane Nane 2017 kufikisha elimu kwa wananchi ili kuzuia ukatili na unyonyaji dhidi ya watoto hao.

Katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Ziwa yanayofanyika uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza, pamoja na mambo mengine, pia shirika hilo linatoa elimu ya ufahamu kuhusu mfanyakazi wa nyumbani, haki zake, wajibu wake, wajibu wa mwajiri wa mfanyakazi wa nyumbani sheria na mikataba inayomlinda mfanyakazi wa nyumbani lengo ikiwa ni pamoja na kuimarisha haki, ulinzi na fursa kwa mtoto mfanyakazi wa nyumbani.

Aidha katika banda la WOTESAWA, kuna kazi za aina mbalimbali zilizotengenezwa na watoto wafanyakazi wa majumbani chini ya shirika hilo.

Fika banda la WOTESAWA kwa elimu zaidi, ama pia simu nambari 08 00 71 00 66 bure kwa taarifa zozote za ukatili dhidi ya wafanyakazi wa nyumbani.

Baadhi ya wadau wa usalama wakiwa kwenye banda la WOTESAWA kwenye Maonyesho ya Nane Nane Nyamuhongolo Jijini Mwanza

Banda la Shirika la WOTESAWA

BMG Habari, Pamoja Daima

Recommended for you