Audio & Video

Kamati ya Siasa Mkoa Mwanza yakagua miradi ya maendeleo Halmashauri ya Buchosa

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa Mwanza (CCM) leo wametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya na maji katika halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo kama Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/10 inavyoelekeza.

Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Dkt.Antony Diallo wameridhishwa na uboreshaji wa Kituo cha Afya Kome kinachotekeleza mradi wa ujenzi wa majengo ya upasuaji, maabara, wodi ya wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti pamoja na nyumba mbili za watumishi ambao umefikia katika hatua nzuri ukigharibu shilingi milioni 400 zilizotolewa kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi (RBF).

Upanuzi Kituo cha Afya Kome kilichopo Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema ambapo upanuzi huu utasaidia wananchi kupata huduma za afya karibu badala ya kwenda Mjini Sengerema

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella ambaye pia ni Mjumbe Kamati ya Siasa (CCM) Mkoa Mwanza

 

 

SOMA Halmashauri ya Misungwi yapongezwa na Kamati ya Siasa Mkoa Mwanza

Recommended for you